Breaking News

Diamond Platnumz afikisha watazamaji milioni 900 Youtube

Monday March 23 2020

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz amefikisha watu milioni 903 waliotazama kazi zake mbalimbali katika mtandao wa Youtube hadi leo Jumatatu Machi 23, 2020 saa 7 mchana.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul alijiunga na mtandao huo Juni 12, 2011 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.

Diamond katika akaunti yake ya Youtube tayari ana wafusi 3.28 million akiwa msanii wakwanza Tanzania kuwa na wafuasi wengi katika mtandao huo.

Baadhi ya matukio anayoyaweka katika mtandao huo ni shoo anazozifanya ndani na nje ya nchi, matangazo ya bidhaa na huduma, matukio ya kijamii anayoshiriki na utayarishaji wa video za nyimbo zake.

Mbali na hilo pia amekuwa akiweka picha mnato anazopiga akiwa peke yake au na watu wake wa karibu, wakiwemo baadhi ya mashabiki zake wanaocheza nyimbo zake mbalimbali.

Mathalani wimbo  Yope aliyoshirikishwa na msanii Innos’ B wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umetazamwa mara milioni 73 ndani ya miezi sita, kuwa wimbo unaoongoza kwa kutazamwa zaidi.

Advertisement

Kutokana na idadi hiyo ya watazamaji, Diamond amewaacha mbali wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki akiwemo msanii Wizkid mwenye watazamaji milioni 792.

Davido ana watazamaji milioni 543 na Burnaboy ana watazamaji milioni  429.

Tangu alipoanza muziki miaka 10 iliyopita, Diamond ameshaachia nyimbo mbalimbali ikiwemo Mdogo mdogo, Nitampata wapi ,Inama aliomshirikisha Fally Ipupa, Number One Remix aliomshirikisha Davido, Nana, African Beauty na Marry you.

 

Advertisement