Hivi ndivyo Linex na Ekothee walivyokutana

Tuesday April 9 2019

 

Wakiwa na siku tano tangu waachie wimbo wa ‘Baraka’ msanii Linex ameeleza mazingira walivyokutana na Ekothee hadi kufika hatua ya kufanya kazi.

Linex iliyewahi kutamba na kibao cha ‘Moyo wa Subira’ alisema miaka miwili iliyopita alimuandikia Ekothee ambaye ni mwanamuziki kutoka Kenya ujumbe mfupi kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na kumjibu mwaka jana.

Katika ujumbe huo pamoja na mambo mengine Linex alimwambia mwanamuziki huyo kuwa anapenda namna anavyoimba nyimbo zake kwa kutumia lugha ya kijaluo.

Naye alimueleza kuwa anapenda nyimbo yake ya Salima na hapo ndipo akamuuliza kwa nini wasifanye kazi pamoja na ndipo wazo la wimbo wa ‘Baraka’ lilipoanzia hadi kufikia kupika kibao hicho.

“Mitandao ya kijamii imerahisha mawasiliano hata mtu asiposoma leo ujumbe wako ipo siku atasoma kwani hata mimi hutumia kusoma maoni ya watu yanayonisaidia kuboresha kazi zangu vivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu na Ekothee kujauna,” alisema Linex.

Advertisement