Advertisement

Nandy afunguka baada ya kuvishwa pete

Sunday April 12 2020
pic nandu

Ikiwa imepita siku moja tangu avalishwe pete ya uchumba, msanii Nandy afunguka kwa mara ya kwanza.
Juzi Jumapili, Aprili 10,2020 Nandy ambaye jina lake halisi ni Faustina Charles alivishwa pete na mchumba wake Billnass ambaye naye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva.
Billnass alifanya tukio hilo wakati Nandy alipokuwa akitumbuiza katika shoo ya kipindi cha Homa inayorushwa na kituo cha TVE.
Tangu kutokea kwa tukio hili Nandy hakuwahi kuongea wala kuandika chochote jambo ambalo watu katika mitandao ya kijamii walihisi labda tukio hilo halikiwa na ukweli wowote.
Hita hivyo leo Jumapili Aprili  12,2020 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Nandy ameandika
'THANK YOU ❤️'.
"Kwanza happy belated birthday mchumba wangu mpenzi Billnass kama nilivyo ikubali hii pete basi nimekubali mazuri na mabaya yako kutoka moyoni hakika wewe ni mwanaume wa maisha yangu.
"Unajua navyokupenda, sina mengi ya kuandika hapa sababu nimeyamaliza yote mbele ya uso wako.Safari ndio kwanza inaanza Mungu wetu ni mkuu sana alituvusha na hata hili tutavuka salama.
"Asanteni wote kwa hongera mlizo nipa na kwa kuangalia pia show ya Homa, tuko pamoja,mbarikiwe sana,Nandy ni mchumba rasmi wa William.William Lymo ni jina halisi la Billnass alilopewa na wazazi wake.

Advertisement