Penzi la Kylie na Travis chali

Wednesday October 2 2019

 

By Alinda Kato, Mwananchi [email protected]

Kylie na Travis waachana baada ya kuwa pamoja kwa miaka miwili na kupata mtoto mmoja.

Kylie Jenner (22) na Travis Scott (28) walianza uhusiano wao Aprili, 2017 ambapo Kylie alipata ujauzito ndani ya miezi michache kisha akajifungua mtoto wao Stormi Februari 2018.

Kwa mujibu wa tovuti ya  TMZ imesemekana wapenzi hao hawajaonekana pamoja hadharani tangu Agosti 27, 2019.

Mara ya mwisho wawili hao kuwa pamoja ni Agosti walipoungana na marafiki na familia kwenye boti ya kifahari nchini Italia wakiadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Kylie.

Kisa cha kuwa mbali kinatajwa ni usaliti wa mapenzi ambapo Kylie anamshuku Travis kumsaliti licha ya kukanusha mara kadhaa.

TMZ katika kulikazia hilo inabainisha kuwa Kylie hajatuma picha yoyote akiwa na Travis tangu Septemba 10, 2019.

Advertisement

Travis hakuonekana kwenye harusi ya Justin na Hailey Bieber mwishoni mwa wiki iliyopita huko South Carolina, ambapo Kylie alihudhuria na mtotoao Stormi.

Kylie alionekana kufurahia harusi akiwa na marafiki kama Jaden Smith ambaye iliwahi kuvumishwa kuwa ni mpenzi wake licha ya kukanusha baadaye kwa madai ni rafiki yake wa miaka mingi

Advertisement