Rapa Cardi B kuongoza tamasha la Unlocks Johannesburg

Sunday February 23 2020

 

Msanii wa Hip hop kutoka Marekani Cardi B anatarajia kuongoza tamasha la Unlocks mwaka huu linalotarajiwa kufanyika TicketPro Dome Jijini Johannesburg Afrika Kusini Juni 12.
Ikiwa ni mara yake ya kwanza, Cardi B  ni moja kati ya wasanii wenye uhitaji na ushawishi mkubwa katika muzikiwa Hip-Hop akiwa na tuzo ya Grammy pamoja na rekodi ya dunia kama msanii wa kike mwenye Nyimbo Nyingi zaidi kwenye ingizo la US Hot R&B/Hip-Hop Top 10 kwa wakati mmoja.
Waandaji wa tamasha hilo Castle Lite wanasema wanayo furaha kubwa kumkaribisha Cardi B kuwa kinara wa tamasha la Unlocks huku pia wakisherehekea mwaka wa 10.
“Huu ni mwaka mkubwa sana kwa chapa ya Castle Lite Unlocks, sio tu kwamba tunasherehekea miaka kumi ya kutoa mchango katika jamii ya Hip-Hop Afrika kuliko chapa nyingine yoyote, lakini pia tuna sherehekea miaka 10 ya kutoa fursa ya kipekee kwa mashabiki wandani wa muziki huu, kuweza kuwaona nyota wao wakubwa kama vile Drake, J Cole, Chance the Rapper, Kanye West, Travis Scott, Post Malone, na Meek Mill. Na sasa uwepo wa Cardi B unatimiza miaka 10 kabambe ya tamasha la Unlocks,” alisema Mkurugenziwa Castle Lite, Silke Bucker.
Tamasha hilo mwaka juzi ilimleta msaani wa hip hop jijini Dar es Salaam na baadaye pia walimleta msaani Nasty C kutoka South Africa.

Advertisement