VIDEO: Seth kuzikwa saa kumi kesho makaburi ya Kinondoni

Sunday December 8 2019

Seth Bosco,Mbezi Temboni,Chama cha Waigizaji Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania,Steven Kanumba ,

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi [email protected]

Msanii Seth Bosco, ambaye alikuwa mdogo wa marehemu Steve Kanumba anatarajiwa kuzikwa kesho saa kumi..

Msemaji wa familia, Novatus Mayenja maarufu kwa jina la Nova ameyasema hayo leo Jumapili, Desemba 8, alipozungumza na Mwananchi kuhusu ratiba ya mazishi kwa siku ya kesho.

Nova amesema mwili utawasili nyumbani kwao Kimara Temboni saa 5:00 asubuhi ukitokea Muhimbili.

"Baada ya mwili kuwasili saa tano ndugu ,jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima zao za mwisho ikifuatiwa na ibada  saa 7:00 mchana,   tutaelekea kanisa la KKKT Temboni ambako kutafanyika misa na kisha kuelekea makaburini kwa ajili ya maziko ambapo tunatarajia kuwepo huko saa 10:00 jioni," amesema Nova.

Seth ambaye pia ni mtunzi wa filamu, amefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwao Kimara Temboni baada ya kuzidiwa ghafla.

Takribani miezi mitatu alikuwa akisumbuliwa na uvimbe katika uti wa mgongo ambapo alifanyiwa operesheni na kuendelea na matibabu na mazoezi akiwa nyumbani.

Advertisement

Hata hivyo siku ya Ijumaa, mama yake Flora Mtegeo, alisema  hali yake ilibadilika ghafla ambapo alifariki saa 6:30 usiku

Advertisement