Mama yake kocha wa zamani Nigeria atekwa

Monday July 15 2019Ogere Siasia

Ogere Siasia 

By AFP

Port Harcourt, Nigeria. Watu wenye silaha leo wamemteka mama wa kocha wa zamani wa soka wa Nigeria, Ogere Siasia na ndigi zake wamesema utekaji katika siku za karibuni unawalenga wanamichezo nyota.
Beauty Ogere Siasia alitekwa akiwa nyumbani kwake katika jimbo la kusini la Bayelsa na watu wawili majira ya saa 8:15, ndugu yake, Olotu Frederick aliiambia AFP.
Utekaji watu kwa nia ya kutaka kupewa fedha nyingi ni kitu cha kawaida nchini Nigeria, hasa katika majimbo ya kusini ambako matajiri wa Kinigeria na wafanyakazi wageni wamekuwa wakitekwa wakati wa vipind vya fujo. Wamekuwa wakitekwa na wapiganaji ambao wanataka mgawo mkubwa zaidi katika mapato ya mafuta ghafi.
Ndugu wa wanamichezo maarufu pia wamekuwa wakiwindwa na makundi hayo.
Baba wa nahodha wa zamani wa tiomu ya taifa, John Mikel Obi pia alitekwa mwaka jana akiwa mji wa Enugu ulio kusini mashariki kabla ya watekaji kulipwa fedha na kumuachia.
Awali mama huyo wa Siasia alitekwa mwaka 2015 na kushikiliwa kwa siku 13 kabla ya fedha kulipwa na baadaye kuachiwa.
Siasia alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ambaye baadaye aliteuliwa kuwa kocha kwa vipindi viwili; mwaka 2010 na 2016.

Advertisement