Askofu mstaafu Mmole afariki dunia, kuzikwa Mei 21

Wednesday May 15 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Askofu mstaafu, Gabriel Mmole wa Jimbo Katoliki la Mtwara amefariki dunia leo alfajiri Mei 15, 2019.

Taarifa  za kifo hicho zimetolewa leo na katibu mkuu wa  Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima.

Akizungumza na Mwananchi Kitima amesema askofu Mmole amefariki akiwa na umri wa miaka 80, kwamba alikuwa mgonjwa.

“Mazishi yatafanyika Mei 21, 2019 mkoani Mtwara,” amesisitiza Padri Kitima.

Advertisement