Chakachaka atua tamasha la ZIFF

Wednesday July 10 2019

Chakachaka tamasha, ZIFF, Yvonne Chakachaka,Zanzibar Tanzania,

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Zanzibar. Mwanamuziki  Yvonne Chakachaka ametua kisiwani Zanzibar nchini Tanzania katika tamasha la 22 la Filamu za Zanzibar (ZIFF) atakakofanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja kushiriki  kongamano la wanawake.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa masoko wa ZIFF, Isihaka Mlawa mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wageni maalum mwaka 2019 watakaofanya shughuli za kijamii.

“Amewasili jana na leo ataendelea na programu maalum ikiwemo kukutana na wanafunzi wanaopata mafunzo ya filamu na wasanii wa muziki kutoka Chuo cha Muziki cha Dhow Country Music Academy,” amesema.

Amesema mwanamuziki huyo na aliyeimba wimbo wa Zanzibar miaka 40 iliyopita, Sipho Mabuse watafanya shoo ya muziki katika tamasha hilo linaloendelea visiwani Zanzibar.

Chakachaka ametamba na nyimbo mbalimbali kama, I'm Burning Up, I'm in Love With a DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland na Umqombothi.


Advertisement

Advertisement