Matokeo kidato cha nne 2018 haya hapa

Muktasari:

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40


Dodoma. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.

Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).

Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.