Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Mstaafu auawa kikatili Dar

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limethibitisha kifo cha Tunsume Sakajinga, mkazi wa wilayani Temeke jijini Dar es Salaam  anayedaiwa kuuawa na mfanyakazi wake wa ndani.

Dar es Salaam. Tunsume Sakajinga (60), mkazi wa wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ameuawa baada kupigwa na kitu kizito kichwani kisha kuchomwa na mkasi shingoni na mtu anayedaiwa kuwa kijana wake wa kazi za nyumbani.

Msemaji wa familia ambaye ni kaka wa marehemu, Kisa Mwankusye amelieleza Mwananchi kuwa mauaji hayo yametokea juzi Januari 12, 2019 saa tano asubuhi na kwamba marehemu alikutwa amechomwa mkasi shingoni na kupigwa na kitu kizito kichwani.

“Tulipata taarifa hizo saa tano asubuhi, jambo hili linaumiza sana kwa sababu lipo chini ya mikono ya polisi tunawaachia wao,” amesema Mwankusye.

Amesema dada yake alistaafu Desemba 31, 2018 na kwamba nyumbani alikuwa akiishi na kijana huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke,  Emmanuel Lukula amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo lakini amesema bado wanafanya uchunguzi kubaini nani alihusika na kwamba hakuna mwenye uhakika kama aliuawa na mvulana wake wa kazi.

“Hilo bado tunachunguza na hakuna mwenye uhakika kama ‘houseboy’ wake ndiye alimuua. Siwezi kuthibitisha ila bado tunachunguza,” amesema.