Lema adai kutekwa kwa Mo Dewji kutaporomosha uchumi wa Tanzania

Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema 

Muktasari:

Wakati familia ya mfanyabiashara Mo Dewji ikitangaza donge nono la Sh1bilioni kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwake, Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema amedai tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo  litasababisha kuporomoka kwa uchumi Tanzania


Dar es Salaam. Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema amedai tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji  ‘Mo Dewji’ litasababisha kuporomoka kwa uchumi nchini.

Amesema kutokana na tukio hilo wawekezaji watakuwa na hofu ya kuendelea kuwekeza hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 16, 2018 Lema amesema tukio hilo na mengine yaliyokwisha tokea yanazua hofu miongoni mwa wawekezaji ambao huenda wakakimbilia nchi jirani.

“Watu wenye capital (mitaji) wataondoa mitaji yao watakwenda nchi zenye usalama. Watu wataogopa watoto wataanza kutekwa, familia zitaanza kusumbuliwa na kwa sababu haya matukio yamekuwa ni mfululizo,” amedai Lema.

Lema amesema mbali na familia ya Dewji kutangaza dau kwa atakayesaidia uchunguzi wa tukio hilo bado familia ina uwezo wa kuajiri wapelelezi binafsi wa kimataifa huku akiitaka Serikali kuruhusu wapelelezi binafsi.

Soma zaidi: