Mamelodi wakwama kwa Azam

Thursday February 02 2017
mamelodi

Dar es Salaam.Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini  wameshindwa kufurukuta mbele ya Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Taifa usiku huu.

Mamelodi ambao wapo nchini kwa ziara ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu nchini Afrika Kusini na mchezo wa Super Cup dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa mwezi huu, licha ya kutawala muda mwingi wa mchezo walishindwa kupenya ngome imara ya Azam iliyoongozwa na nahodha Himid Mao.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Sundowns, Pitso Mosimane alisema kuwa Azam FC walikuwa kipimo bora kwao kutokana na kiwango walichoonyesha.

“Nawapongeza vijana wangu kwa kucheza vizuri na nimeridhika na kiwango chetu ingawa sijafurahi kwa sababu hatukufunga bao. Pia niwapongeze Azam kwa kucheza vizuri na walionyesha kiwango bora uwanjani,” alisema Mosimane.

 

 

Advertisement

 

Advertisement