Waliokufa Ziwa Victoria wafikia 12

Monday October 09 2017
pic ajali

Idadi ya watu waliokufa baada ya Toyota Hiace kuzama Ziwa Victoria imeongezeka na kufikia 12.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu amesema katika ajali hiyo watu watatu wameokolewa wakiwa hai.

Msangi amesema walionusurika wameokolewa na wananchi ambao ni wataalamu wa kuogelea.

Soma : Hiace yakatisha maisha ya watu wanane Ziwa Victoria

Advertisement