Muungano wa Tigo na Zantel utakuza uchumi nchini

Thursday July 11 2019

 

Dar es Salaam, IMEELEZWA kwamba kuungana kwa kampuni za simu za mkononi Tigo na Zantel kutaoboresha sekta ya uchumi na mawasiliano nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa jarida la Forbes Africa Tanzania inatarajia kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wakati, uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 na sekta ya mawasiliano imekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha hilo.

limesema Sekta hii imeleta mapinduzi makubwa katika maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano na matumizi ya huduma ya fedha kwa njia ya simu.

Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za mwezi Desemba 2018, jumla Watanzania milioni 43.5 wanatumia mitandao mbalimbali ya simu.

Mkurugenzi wa Tigo Siomon Karikari katika mahojiano na jarida hilo alisema kuwa kati ya mwaka 2009 hadi 2017 idadi ya Watanzania wanaotumia huduma rasmi za kuweka, kutuma na kupokea fedha imeongezeka kutokana na kukua kwa huduma hizo kupitia simu za mkononi.

Hii ni hatua nzuri kwani kwa kuangalia taarifa ya Tanzania National Financial Inclusion Framework 2018-2022 tunaona kuwa asilimia 55 ya Watanzania hawakuwa katika mfumo rasmi wa kutuma, kupokea na kuhifadhi fedha  muongo mmoja uliopita.

Advertisement

Naye Kaimu mkurugenzi wa Zantel Brian Karokola katika mahojiano na jarida hilo alisema Ili kuhakikisha kuwa sekta hii ya mawasiliano inaendelea kukua na kuboresha maisha  ya wananchi ni lazima mazingira rafiki kwa ukuaji wa sekta hii yatengenezewe.

Kwa hali ilivyo sasa kuna jumla ya watoa huduma nane wa mawasiliano ya simu za mkononi ambao wanashinda katika soko la Tanzania. Uimarishaji wa soko unashauriwa kuwa ndio njia pekee ya kuelekea mbele na kuleta maendeleo.

Hivyo wamewataka watanzania kujitokeza kwa wingi na kuunga mkono juhudi hizo ili kampuni hizi mbili ziweze kufanikisha dhamira yake ya kutengeneza soko imara na lenye ubora katika sekta ya mawasiliano litakalokuwa na tija na manufaa maradufu kwa wote.

Advertisement