Mapya yaibuka ndege ya Boeing 737

Thursday February 20 2020

 

Washington, Marekani. Utafiti mpya uliofanywa katika ndege za Boeing 737 Max umebaini kuwa bado si salama.

Utafiti huo umebaini kuwa kuna virusi vinavyopatikana katika matanki ya mafuta katika ndege kadhaa ambazo zilikuwa zinasubiri kuwasilishwa kwa wanunuzi.

Taarifa ya msimaizi wa ndege hiyo ilisema kwamba ugunduzi huo ni jambo lisilokubalika.

Mmoja wa wasemaji wa shirika la Boeing aliliambia Shirika la utangazaji la BBC kwamba kampuni hiyo haikugundua tatizo hilo na kusababisha ndege hizo kuchelewa zaidi kuanza tena huduma zake.

Tatizo hilo limekuja wakati ambako ndege aina ya 737 Max ikiwa bado haijaidhinishwa kurejea kutoa huduma baada ya kusababisha ajali mbili mbaya zilizopoteza maisha ya abiria wote.

Shirika hilo la Marekani lilisema kwamba limegundua vifusi vilivyoachwa ndani ya matanki ya mafuta katika ndege ambazo hazijawasilishwa kwa wateja wake kama ilivyokusudiwa.

Advertisement

“Wakati tunazikagua na kuchunguza ndege za 737 Max vile zilivyo kabla ya kuziwasilisha, tukagundua virusi,” ilisema taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilisema kwa sasa kampuni hiyo imeanzisha uchunguzi mpya na wakina pamoja na kufanyia mfumo wake marekebisho mara moja.

Advertisement