Migahawa miwili Japan kileleni mwa hoteli bora duniani

Muktasari:

Orodha ya La Liste huzipanga hoteli kwa ubora kwa kuzingatia wastani wa nafasi zinazoshika katika uchambuzi wa taasisi tofauti, magazeti na tovuti.

Migahawa miwili ya Japan imepanda hadi kileleni mwa orodha ya ubora duniani ya La Liste, huku ya tatu ikishika nafasi ya pili katika orodha ya "guide of guides".
Mgahawa wa Sugalabo wa jijini Tokyo unaomilikiwa na Yosuke Suga, ambao una meza 20 tu, hauna nyota ya ubora wa Michelin-- orodha ya hoteli kwa kuzingatia ubora-- lakini unashika nafasi ya juu ya orodha hiyo inayoandaliwa na taasisi ya Ufaransa sambamba na Guy Savoy ya Paris na Le Bernardin ya New York.
Mgawa unaojulikana kwa ubunifu wa Ryugin ambao upo Tokyo na unaoendeshwa na Seiji Yamamoto uliruka kwa nafasi 30 hadi kileleni kuungana na migahawa hiyo mitatu.
Mgahawa wa Kitcho Arashiyama ulioko Kyoto ni mmoja kati ya hoteli saba, ikiwemo ya Alain Ducasse ya Monaco zilizochangia nafasi ya pili.
Hoteli ya Plaza Athenee ya Paris inayopendwa na watu maarufu, imeshika nafasi ya nne katika orodha hiyo ambayo huchukua wastani wa uchambuzi wa taasisi tofauti, magazeti na mitandao, ukiwemo wa TripAdvisor.
Lakini kupanda kwa kasi kwa Suga, 43, ambaye wakati fulani alikuwa msaidizi binafsi wa mpishi maarufu wa Ufaransa, Joel Robuchon, ndiko kunaweza kuvutia wengi.
Mwaka jana Sugalabo haikuweza hata kuingia katika orodha ya hoteli 1,000 bora ya La Liste.
Hoteli hiyo hufungwa kwa siku kadhaa kila mwezi kumuwezesha Suga kuzunguka ili apate wazo jipya na viungo.
Ingawa anatokea katika familia ya wapishi ambao wamesomea utamaduni wa Kifaransa, chakula chake ni cha asili ya Kijapani.