Wakenya waongezeka kwa milioni tisa

Muktasari:

Takwimu za sensa ya watu ya mwaka 2019 inaonyesha sasa Wakenya wamefikia 47.5 milioni katika kipindi cha muongo mmoja.

Nairobi, Kenya. Idadi ya watu nchini Kenya imeongezeka kwa milioni tisa katika kipindi cha muongo mmoja.

Kwa mujibu wa sensa ya watu iliyofanywa mwaka 2019, idadi ya Wakenya imefika 47,564,296 ukilinganisha na 38.6 milioni ya mwaka 2010.

Tovuti ya Gazeti la The Daily Nation la Kenya imeandika kuwa idadi hiyo inaonyesha kwamba wanawake ni wengi ukilinganisha na wanaume.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Kenya (KNBC), imetoa ripoti ya sensa hiyo leo Jumatatu Novemba 4 katika ghafla iliyofanyika ikulu jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Rais, Uhuru Kenyatta maeneo ambayo yeye  idadi kubwa ya watu ni pamoja na mji mkuu wa Nairobi, Kiambu, Nakuru, Kakamega, Bungoma, Meru na Kilifi.

“Nairobi ina watu 4.4 milioni karibu mara mbili ya watu wanaopatikana katika miji ya Kiambu na Nakuru yenye wakazi zaidi ya milioni mbili,” ilisema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ilisema kuwa watu wengie milioni 15 wanapatikana katika mikoa ya  Kakamega yenye wakazi zaidi ya milioni moja ikiongozwa na Kakamega (1.87 mil), Bungoma (1.67 mil), Meru (1.54ml) na Kilifi (1.45 ml).