Wanaousaka urais, ubunge CCM kabla ya wakati waonywa

Tuesday December 3 2019

 

By Muhammed Khamis, Mwananchi [email protected]

Pemba. Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewaonya wanachama wa chama hicho tawala walioanza mikakati ya kusaka kupitishwa kuwania udiwani, ubunge na urais akibainisha kuwa kufanya hivyo ni makosa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 3, 2019 katika ziara yake kisiwani Pemba, Zanzibar wakati akizungumza na kamati ya siasa Wilaya ya Chakechake.

Dk Bashiru amesema watu wa namna hiyo hawatavumiliwa kwa kuwa taratibu za kuwania uongozi, nafasi mbalimbali katika chama hicho zipo wazi na zina muda wake.

Katibu mkuu huyo amesema wana taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wameanza kampeni mapema wakilenga kuchaguliwa jambo ambalo halikubaliki.


Advertisement