Aliyekuwa kiongozi wa CCM Dodoma kufikishwa mahakamani na mwenzake

Wednesday March 25 2020
kada ccm pic

Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo Jumatano Machi 25, 2020 itamfikisha mahakamani aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Robert Mwinje (39) na muhudumu wa ofisi hiyo Nyemo Malenda (20) kwa makosa matatu.
Mwinje na mwenzake watafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma kwa madai ya kula njama, kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo yote yakiwa ni kinyume na Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema uchunguzi wao umeonyesha kwamba kati ya tarehe 18 na 20 Oktoba 2019 Mwinje akiwa katika nafasi hiyo na muhusika wa ofisi hiyo walighushi barua ya uteuzi wa waomba uongozi ndani ya chama.
Kibwengo amesema walighushi barua hiyo wakijifanya kuwa imetokea na uongozi wa CCM Wilaya ya Dodoma na kuikabidhi kwa mwananchama mmoja kwa hatua huku wakifahamu kuwa ni uongo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Advertisement