Darasa la saba Dar kufanya mitihani kesho, Necta yatoa ufafanuzi

Wednesday January 15 2020Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde 

Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde  

By Elizabeth Edward, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetoa ufafanuzi kuhusu mitihani itakayofanyika kesho Alhamisi Januari 16, 2020 jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wa darasa la saba.

Mtihani huo utahusisha shule zote za umma na binafsi na utafanyika kwa siku moja ya kesho.

Limesema mitihani hiyo ni mazoezi ya ndani ya wanafunzi katika shule za Mkoa huo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Januari 15, 2020 katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kinachofanyika kesho si mitihani ya Necta,  ni jaribio kwa walimu wa Mkoa huo baada ya kupewa mafunzo ya namna bora ya kutunga mitihani.

“Hawana mtihani kama watu wanavyotaka kupotosha, usahihi ni kwamba watakuwa na mazoezi ya ndani ya shule zao ambayo yatasimamiwa na Necta.”

 “Tuliwapa walimu mafunzo ya namna bora ya kuwapa mitihani na mazoezi wanapokuwa shuleni kuhakikisha ufaulu  unakuwa vizuri zaidi na wanafunzi wanaizoea mitihani ya Taifa na kuwa tayari watakapokutana nayo,” amesema Msonde.

Advertisement

Amesema lengo la mazoezi hayo ni kuhakikisha walimu wa shule zote za msingi wanakuwa na umahiri wa kutunga mtihani.

“Tunaamini shule zikiimarika Taifa linaimarika, tunataka ubora wa maswali uongezeke ili wanapofika kwenye mtihani wa mwisho wawe wamebobea. Tunataka tuone kama kuna chochote wamekipata kwenye mafunzo yetu na kama kuna shida tuone ni namna gani tunaweza kuweka sawa,” amesisitiza Msonde

Advertisement