Dk Bashiru kufunga mitambo majimbo ya wapinzani Dar

Thursday August 22 2019

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi,CCM,Tanzania,Dk Ally Bashiru ,upinzani wapinzani,

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dk Ally Bashiru  

By Bakari Kiango, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Ally Bashiru amesema atafanya ziara katika majimbo manne ya upinzani mkoani Dar es Salaam akiwataka wajiandae kwa kuwa anakwenda kufunga mitambo.

Majimbo hayo na wabunge wake katika mabano ni Kawe (Halima Mdee), Ubungo (Saed Kubenea), Kibamba (John Mnyika). 

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo leo Alhamisi i Agosti 22, 2019 wakati akizungumza na vijana wa timu ya mpira wa miguu ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) wilayani Temeke ambao ni mabingwa wa michuano ya Sports Extra Ndodo CUP.

“Nilitamani kukaa nanyi kwa muda mrefu lakini kutokana na majukumu ya kazi sitoweza. Nina mambo manne ya kuzungumza nanyi.”

"Mambo haya nitayazungumza pia kwenye ziara yangu ya majimbo ya Kawe, Kibamba na Ubungo. Nataka nikafunge mitambo ya kushambuliwa wapinzani wetu," amesema Dk Bashiru.

Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam na katika ujumbe wake kwa vijana hao, Dk Bashiru amewataka kuwa wazalendo, kulinda rasilimali, kuchagua viongozi bora wenye uadilifu na wasikubali kutumika kwenye michezo.

Advertisement

 


Advertisement