Jalada kesi ya mfanyabiashara Hariri lipo kwa DPP

Muktasari:

  • Jalada la kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mfanyabiashara Hariri Mohamed Hariri, liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kupitiwa, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa leo Januari 2, 2019

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mfanyabiashara Hariri Mohamed Hariri, liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kupitiwa, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa leo Januari 2, 2019.

Wakili wa Serikali, Esther Martine ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega leo na kuomba shauri hilo kupangiwa tarehe nyingine.

Hakimu Mtega baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, 2019 huku mshtakiwa huyo akirejeshwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.

Katika kesi ya msingi, Hariri anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 2, 2018 Kinondoni Matitu, Dar es Salaam.

Anadaiwa siku ya tukio alikutwa akisafirisha gramu 214.11 za heroin.