VIDEO:Nyoka aliyezua gumzo Chato apelekwa kuhifadhiwa

Wananchi wakiwa wamembeba nyoka aina ya Chatu anaedaiwa kuwa wa bahati kutokana na upole wake aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato

Muktasari:

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa) imemchukua nyoka mkubwa aina ya chatu aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Chato. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania (Tawa) imemchukua nyoka mkubwa aina ya chatu aliyeonekana katika kijiji cha Kasala kata ya Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Chato,  Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi wilayani Kahama kuhifadhiwa.

Nyoka huyo anayeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 11, 2019 amesema Tawa iliwatafuta wataalam wa nyoka kutoka makumbusho ya Bujora waliofanikisha kumchukua noka huyo aliyekuwa katika kichuguu akiwa amelalia mayai 20.

Mmoja wa Wananchi wa kijiji hicho,  Philipo Maduhu amesema nyoka huyo ni baraka kwao na halmashauri haikupaswa kumuondoa.