VIDEO: Makonda kuhamasisha maandamano Dar

Friday October 04 2019
makondapic

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema atahamasisha maandamano ya wakazi wa kata tano wilayani Ilala kwenda wizara ya Tamisemi ikiwa ujenzi wa mifereji eneo la Buguruni Mivinjeni hautaanza ifikapo Oktoba 10, 2019.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Ilala baada ya kupewa majibu yasiyoridhisha na Emmanuel Ndyamukama,  mratibu wa miradi ya uboreshaji  wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) wa Tamisemi aliyekuwa akizungumza naye kwa simu.

Katika majibu yake Ndyamukama amesema mradi huo haujakwama na kilichofanyika sasa ni makubaliano kati ya Wizara ya Fedha na Mipango na Tamisemi.

“Tuna miezi sita bado wanajiridhisha nini, mvua zinakuja. Hapa tuna mifereji na wewe (huyo mtendaji) shahidi nimepigia kelele muda mrefu. Wananchi hawamjui anayehusika zaidi ya Rais, makamu wa rais, waziri mkuu na jumba bovu linamuangukia mkuu wa Mkoa.”

Makonda: Kama siyo njaa ningejiuzulu

“Naomba jambo moja, leo ni Oktoba 4 na ikifika Oktoba 10 kama mkandarasi hajaanza na mifereji hii ipo nahamasisha maandamano ya kata zote tano tunakuja huko ofisini kwenu. Mwambie bosi wako, katibu mkuu Tamisemi na waziri wa Tamisemi kwamba tunakuja na kata zote tano,” amesema Makonda.

Advertisement

VIDEO: Makonda aja na jambo jipya Dar

Ameongeza, “Haiwezekani tusaini mkataba na kuingia makubaliano na kuahidi wananchi halafu bado kazi haifanyiki. Tunaobeba mizigo ni sisi, hao wote wakifika wanaona Makonda ameshindwa kazi kumbe mpo mlioshindwa kazi, hivi kutoka Tamisemi hadi Wizara ya Fedha mnatumia muda gani?”

VIDEO: ‘Makonda anajihujumu mwenyewe’


Advertisement