Watano kesi ya bomba la mafuta wafutiwa mashtaka, waachiwa huru

Muktasari:

  • Kwa mara ya kwanza, washtakiwa wote 11, wakiwemo watano walioachiwa huru walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Januari 16, 2018 kujibu mashtaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA).

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa watano waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA).

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Septemba 23, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Walioachiwa huru ni  Audai Ismail (43) Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Endelea kufuatililia Mwananchi kwa taarifa zaidi