Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Billnass azikingia kifua tuzo za TMA, agusia ishu ya Darasa

Muktasari:

  • Lakini licha ya kuwa mwanamuziki wa Hip-hop nchini Darasa kutotajwa kwenye kipengele cha Mwimbaji Bora wa Hip-hop, lakini Billnass amesema msanii huyo anafaa kwenye kipengele hicho kwani kwa mwaka jana ametoa nyimbo nyingi ambazo zilifanya vizuri.

Dar es Salaam, Mwanamuziki William Lyimo maarufu kama ‘Billnass’ amesema tuzo zote duniani huwa zinalalamikiwa hivyo kwa maoni ambayo yanaendelea kutolewa dhidi ya Tuzo Za Muziki Tanzania (TMA) yasiwe ya kuvunja moyo.

Billnass ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari jana Septemba 3, 2024 kwenye usiku wa kutambulisha wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Nandy Festival Kigoma.

"Mimi niipongeze Serikali, wizara husika, na wadau tumekaa kipindi kirefu hatuna tuzo kwa hiyo makosa ambayo yanaonekana ni katika kujifunza tuzo zote duniani huwa zinalalamikiwa kuna makosa yapo yanaonekana na mengine kila mmoja anaona kwa namna yake sitamani kuona hakuna tuzo kwa hiyo tusiwavunje moyo tusifanya kuonekana kama hakuna kinachofanyika,”amesema Bilnass.

Licha ya kuwa mwanamuziki wa Hip-hop nchini Darasa kutotajwa kwenye kipengele cha Mwimbaji Bora wa Hip-hop katika tuzo hizo amesema msanii huyo anafaa katika kipengele hicho.

"Nawapongeza wasanii wote walioingia kwenye 'nominations' mfano kwa mwanamuziki kama Darasa huwa anafanya vizuri sana 'No Body' aliofanya na Bien ukiangalia kwa namba na namna ambavyo imepokelewa kwa hiyo mtu kama yule kwangu mimi anafaa kwenye tuzo na hata ukiangalia kwenye orodha ya wasanii bora wa hip-hop huwa yupo.

"Lakini hata walioingia kwenye vipengele wanastahili maana sidhani kama kuna mtu ambaye hastahili,"amesema Billnass na kumalizia kuwa alitamani pia kumuona Jux kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kiume lakini hajamuona.

Ikumbukwe kuwa kamati ya uandaaji wa tuzo hizo za (TMA) ilitangaza majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo katika kipengele cha Msanii Bora wa Kiume wa mwaka. Ambapo katika majina hayo lipo la Marioo wimbo wa ‘Shisha’, Diamond ‘Shu’, Harmonize ‘Single Again’, Ali Kiba ‘Sumu’ na mwisho ni Jay Melody na wimbo wa ‘Nitasema’.

Huku upande wa Mwimbaji Bora wa Hip-hop akitajwa Joh Makini (Bobea), Kontawa (Dunga Mawe), Rosa Ree (Mama Omollo), Stamina (Machozi), na Young Lunya (Stupid).