Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Marioo mwendo wa kuvimbiana

Muktasari:

  • Naweza kukutajia mastaa wengi wakubwa Bongo hii. Ambao siyo hawana vipaji, bali hawajulikani wanafanya shughuli gani. Lakini ni staa mkubwa. Ustaa wa kweli unaenda na pesa. 

Dar es Salaam. Staa yeyote hajawa staa mkubwa kwa bahati mbaya. Ustaa tofauti sana na kipaji. Unaweza kuwa na kipaji usiwe staa. Na unaweza kuwa staa mkuwa bila kipaji. Yes ndiyo ukweli. 

Naweza kukutajia mastaa wengi wakubwa Bongo hii. Ambao siyo hawana vipaji, bali hawajulikani wanafanya shughuli gani. Lakini ni staa mkubwa. Ustaa wa kweli unaenda na pesa. 

Staa njaa njaa njaa? Siyo staa huyo ni binadamu anayejulikana tu. Anajulikana kwa uso, kazi au umbile kama siyo sehemu kule atokako. Siyo kila ajulikanye ni staa hapa duniani.

Kuna watu hulazimisha ustaa bila kupitia njia sahihi. Hao wanaishia kuwa kituko. Kuna wanaostahili kuwa mastaa ila ‘laifu staili’ yao inawakataa. Wanabaki kuwa ni binadamu wa kawaida.

Ustaa hujengwa na mhusika mwenyewe au watu wake. Staa anaandaliwa na yeye hujiandaa kuwa staa mkubwa. Wapo pia ambao ustaa unamfuata bila yeye kujiandaa.

Omary Mwanga, kazaliwa miaka 30 iliyopita. Ni mwaka 1995, huko kitaa cha Temeke. Wakati Mzee Kihiyo akiwa ‘bize’ kutaka Ubunge wa Tmk. Dogo alikuwa anazaliwa kuja kukiwasha duniani.

Mama Omar hakudaka ujauzito ili ajifungue mtoto staa wa muziki. Alidaka ujauzito ili ajipatie mtoto. Haya ya mbeleni hakuyajua, leo hii mtoto wake, aliyempa jina la Omar ni staa wa muziki. 

Ni mtunzi na mtayarishaji wa nyimbo. Alilelewa ‘bushi’ na bibi yake Kibiti huko. Ndiko alikokulia mtoto wa Kindengereko. Wakati mamaake akimpa jina la Omary, Bongo Fleva inamwita Marioo.

Marioo alianza ‘gemu’ la muziki kama mtunzi wa nyimbo. Alitunga dude kama Wasikudanganye, pini la Nandy. Kuna lile la Unaniweza, alioimba Jux. Hapa alikuwa kama utumbo ndani ya tumbo.

Ghafla akawa mkubwa madude kama ya maana la ‘Bia Tamu’.
Likampa tuzo ya TMA kama wimbo bora wa mwaka 2021 na 2022. Hapa ndipo dogo akaleta balaa zaidi. Kutoka kuwa wa kawaida hadi staa mkubwa.

Alianza na pini la Dar Kugumu. Baada ya hapo ikawa ‘baki tu baki’, ngoma kama Inatosha, Unanionea, Aya, Raha, Chibonge, Salio, Lonely, Unanichekesha, Mama Aminah, Hakuna Matata, na Bia Tamu. 

Wangapi walikuwa wanajitafuta na Marioo 2017? Leo wako wapi wakati Marioo akipata hata ujasiri wa kujiita Mwanamuziki Namba Moja Tanzania? Jeuri hiyo inakuja kwa hisani ya mikono yake.

Dogo kila dude akiachia linaenda safari ndefu. Kila pini linabeba kijiji cha watu. Msitu wa raia na upendo wa tani nyingi. Kwanini? Amejipata na anajua nini afanye kwa ajili ya ‘pipo’ zake. 

Wakati anaanza kuna njia alikuwa akipita. Wenye akili waliona huyu dogo mtu. Alijua ‘kujipozisheni’, alijua akae eneo gani iwe rahisi kwake kutupia nyavuni. Kimsingi hata kujiweka kwa Paula kwake ni bao.

Staa siku zote hutengenezwa na yeye hujitengeneza. Namna yeye anavyosukuma mambo yake ni wazi utaona tofauti kati yake na wenzake. Kuna ‘taimu’ napata shida kujua Marioo na Rayvanny yupi mkubwa. 

Siyo kiumri bali kisanaa. Pia kuna ‘taimu’ nawaza ingekuwaje kama Marioo angekuwa ‘Dabiliuusibii’? Ama kusapotiwa kinguvu kama Mondi kwa Barnaba ama Jux? Ni kwamba Marioo ana njia zake.

Lakini kajikuta katika meza moja na wenzake walioshikwa mkono. Wapo waliosapotiwa na wasanii wakubwa. Wapo waliosapotiwa na media kubwa. Lakini mpaka sasa sielewi ni nani yupo nyuma ya mishe za Marioo. 

Ustaa siyo bahati. Huwezi kuwa staa kwa bahati iwe mbaya ama nzuri. Ustaa siyo jambo kama la kubahatisha. Staa hutengenezwa na yeye kujiwekea mazingira ya kutengenezeka. Marioo pale siyo bahati mbaya. 

Omary kwa sasa kila anachogusa hugeuka dhahabu. Hata Paula amekuwa dhahabu, ana ‘shaini’ bila kiki. Huku mtu wake kila pini likisafiri kilometa nyingi sana. Na ‘baki tu baki’ ya pini baada ya pini na yote ‘hits song’. 

Madogo wanakimbiza njaa katika familia zao. Hawataki watoto zao wakalelewe na bibi zao kwa njaa za wazazi. Wanataka wenyewe ndiyo wawalee watoto na bibi zao. Hasira za ‘laifu’ zikizidi huongeza kasi ya utafutaji. 

Muziki wa Marioo ni Sako la Bako. Anapita wanapopita kwa kasi ya ajabu. Anakisaka kile wao wanakisaka. Hakuna kusubiriana na kuwekeana ratiba kama bodi ya ligi. Toa hits nitoe hits. Toa dude nitoe dude. Mwendo wa kuvimbiana tu.