Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Angel Nyigu: Umaarufu unatesa

Muktasari:

  • Dansa huyo ambaye alipata umaarufu akifanya kazi na lebo ya Wasafi ya Diamond Platnumz na kupitia kazi zake binafsi akiwa mkufunzi wa kudansi, amesema huwa anaishi maisha yake na sio maisha ya watu wengine kuanzia kuvaa hadi kwenye muonekano wa ngozi yake kwenye masuala ya vipodozi.

Dar es Salaam. Wakati wasanii ambao tayari wamejizolea umaarufu kutokana na ukubwa wa kazi walizozifanya wakijitofautisha na mashabiki wao, hili ni tofauti kwa upande wa dansa maarufu Bongo, Angel Nyigu.

Dansa huyo ambaye alipata umaarufu akifanya kazi na lebo ya Wasafi ya Diamond Platnumz na kupitia kazi zake binafsi akiwa mkufunzi wa kudansi, amesema huwa anaishi maisha yake na sio maisha ya watu wengine kuanzia kuvaa hadi kwenye muonekano wa ngozi yake kwenye masuala ya vipodozi.

Ipo hivi, Nyigu amefunguka kuwa umaarufu ni kitu cha kupita na huwa una changamoto kubwa hasa kwenye kuwa huru na maisha yake binafsi na unatesa kwenye uhusiano.

"Katika kitu ambacho kinanitesa kutokana na umaarufu ni kutokuwa huru na maisha yangu, kila mmoja anaishi vile anavyopenda kuishi, hivyo mimi siishi kama wengine, mimi navaa kawaida na huwa sinunui kwa mkupuo kwamba naweza kutaja gharama ikitokea nguo nikaipenda nanunua," amesema.

"Ukitaka kuvaa ukubwa kutokana na umaarufu unakosa uhuru wa kuishi maisha yako, kutokuaminika na jamii au uhusiano na watu kudharaulika na watu kwani unaonekana unajipa ukubwa na kusahau unatokana na mashabiki unaowadharau."

Akizungumzia ratiba yake siku akiwa na shoo amesema huwa  inakuwa ngumu kuanzia asubuhi hadi muda wa tamasha kutokana na kuwa na muda mwingi wa kujiandaa kwa kuhakikisha mambo yake yanakuwa sawa.

"Nikiwa na shoo, ratiba yangu ni ngumu sana, najizingatia mimi zaidi kuliko mtu mwingine kuna muda nakwama hadi kula kwani mambo yanakuwa ni mengi na napenda kuhakikisha kitu changu kinafanyika kwa ukubwa na kinakuwa kizuri.

"Nikiwa sina tamasha huwa ratiba yangu ni kupumzika vizuri, kuangalia movie na wakati mwingine kutoka na watu wangu wa karibu ili kujichanganya nao wasione kama nimewasahau."

Dansa huyo maarufu amekiri kuwa sanaa hiyo kwa namna moja ama nyingine imeweza kumbadilishia maisha yake na anaamini itamfanya aweze kufikia malengo kama alivyoamua kuingia huko baada ya matokeo yake kidato cha nne kutokuwa mazuri akikiri kupata Divisheni Four ya 30.