Ayra uso kwa uso na Rihanna

Muktasari:

  • Wawili hao walipata wasaa wa kuzungumza ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa Riri alimuomba Ayra aingize verse kwenye moja ya ngoma zake.


Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Ayra Starr amekutana na msanii mwenzake Rihanna, usiku wa kuamkia leo katika onyesho la Fenty X Puma lililofanyika jijini London.

Wawili hao walipata wasaa wa kuzungumza ambapo kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa Riri alimuomba Ayra aingize verse kwenye moja ya ngoma zake.

Aidha Rihanna kupitia mahojiano aliyofanya katika onyesho hilo amedokeza kuhusu ujio wa albumu yake ya 9 ambapo amedai kuwa ina hit-song nyingi huku akiwataka mashabiki wake kumpokea tena baada ya kimya cha muda mrefu.

Ili kuonyesha kuwa anamaanisha alichokizungumza Rihanna aliamua kumfollow Ayra kwenye mtandao wa Instagram ambapo mwanamuziki huyo alishindwa kujizuia na kuposti kupitia insta story yake huku akiweka emoji ya machozi.

Endapo ‘kolabo’ hiyo itafanikiwa basi ndoto ya mkali wa ngoma ya ‘Rush’ itatimia kwani kupitia mahojiano yake mbalimbali alikuwa akieleza kuwa anatamani kufanya ngoma ya pamoja na Rihanna kwani ndiye role model wake.

Aidha baada ya wawili hao kukutana bosi wa lebo anayoifanyia kazi Ayra, Don Jazzy, alimpongeza msanii wake huyo kwa kukutana na role model wake huku akiweka wazi kuwa ni kweli Ayra alikuwa akitamani kukutana na Riri na kufanya naye ngoma toka zamani.