Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba mzazi wa msanii Meja Kunta afariki dunia 

Muktasari:

  • Kifo chake kimethibitishwa na meneja wa msanii huyo, Waso Wiso, ambaye ameweka wazi kuwa kwa sasa familia inaanza maandalizi kwa ajili ya mazishi.

Dar es Salaam. Baba mzazi wa msanii wa muziki wa Singeli, Meja Kunta, amefariki dunia leo Julai 21, 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na changamoto za kiafya zinazohusisha presha na kiharusi. Kifo chake kimethibitishwa na meneja wa msanii huyo, Waso Wiso, ambaye ameweka wazi kuwa kwa sasa familia inaanza maandalizi kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza kwa njia ya simu, Waso Wiso amesema madaktari waliwapa taarifa za kifo hicho baada ya juhudi za matibabu kushindikana.

Msiba huo umetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Meja Kunta aeleze hadharani hali ngumu aliyokuwa akiipitia katika kumhudumia baba yake. 

Msanii huyo aliweka wazi kwenye mitamdao ya kijamii kuwa yupo tayari kuuza baadhi ya mali zake ili kupata fedha za kugharamia matibabu, akisema tayari alikuwa ametumia akiba yake yote katika jitihada za kuokoa maisha ya mzazi wake.