Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basata yatoa tamko sakata la Barnaba, Marioo

Muktasari:

  • Baada ya kuwa mvutano kwenye mitandao ya kijamii baina ya wasanii wawili Barnaba na Marioo kuhusu tuzo ya albamu bora 2023 kutotendewa haki, Basata imesema malalamiko hayo hayajawafikia.

Dar es Salaam. Kutokana na mvutano unaoendelea kwenye mtandao wa Instagram kati ya wanamuziki Elias Barnabas, ‘Barnaba’ na Omary Ally,‘Marioo’, kuhusu Tuzo za Muziki Tanzania kutotenda haki Basata imetoa tamko.

Kumekuwa na majibizano kwenye mitandao ya kijamii baada ya Marioo kuwatuhumu waandaaji wa tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kuwa hawatendi haki kwani tuzo ya album bora iliyotolewa 2023, alistahili kushinda yeye.

Mkurugenzi wa Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa ‘Basata’, Edward Buganga akizungumza na Mwananchi leo Mei 21, 2024 amesema utolewaji wa tuzo hizo huzingatia taratibu na kufuata vigezo.

“Hayo ni maoni ya watu, maoni na utaratibu ni vitu viwili tofauti, lakini inapotokea tuzo kuna taratibu zinafuatwa za kuwatunuku watu, kuna vigezo maalumu lazima vinafuatwa kimoja baada ya kingine,” amesema Buganga. 

Ikumbukwe mvutano huo ulianza baada ya Marioo kulalamikia albamu yake ya “The Kid You Know” kutoshinda tuzo na badala yake ikashinda “Love Sounds Different” ya Barnaba kama Albamu Bora Mwaka 2022, ambayo tuzo yake ilitoka 2023.

“Nawauliza waandaaji, kwa nini mnatoa tuzo kama hazitendi haki? Mnaombaje ushauri kwa wanaoshindania? that was not fair at all. Inasikitisha na inakatisha tamaa. This time around jipangeni.

“Albam ya #Tkyk ilikuwa ina hits kubwa, yaani sio ngoma kali tu, hits kubwa zaidi ya 4, lakini cha kushangaza imeshinda albamu ambayo ina hit song moja, sijui mbili na sio kubwa na hit yenyewe niliandika mimi kwenye hiyo albam”. Aliandika Marioo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupelekea Barnaba kumsusia tuzo hiyo. 

Ambapo Barnaba aliandika, "Nimeamua kwenda kubadilisha tuzo hi leo, ku print na nimekuwekea jina lako! Nadhani unastahili so popote uliko nitakuletea au uniambie wapi wakuletee mdogo wangu”.

Kutokana na mvutano huo, Buganga amesema hadi sasa bado wasanii hao hawajafikisha malalamiko yoyote Basata.

“Suala hilo halijafika kwetu, likitufikia kuna utaratibu wa kufanyia kazi, mlalamikaji na mlalamikiwa, tuna wataalamu wa kutosha wa kushughulikia suala hilo, kuna timu ya wanasheria, likifika tutashughulika nalo.
“Lengo letu ni kufanya kazi vizuri na wasanii wote wana haki sawa na Basata ni nyumbani kwao,” amesema.