Basata yazindua 'linki' ya uwasilishaji kazi za wasanii

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari, leo Aprili 19, David Minja ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya tuzo za muziki Tanzania ameeleza kuwa kiungo (link) itakayotumika kuwasilisha kazi za muziki shiriki ni tanzaniamusicawards.com.

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limetangaza mfumo rasmi utakaotumika kuwasilisha kazi katika tuzo za muziki Tanzania (TMA).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Aprili 19, David Minja ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya tuzo za muziki Tanzania ameeleza kuwa kiungo (link) itakayotumika kuwasilisha kazi za muziki shiriki ni tanzaniamusicawards.com.

                      

"Mlango wa uwasilishwaji wa kazi umefunguliwa leo utaenda hadi tarehe 9 Mei, saa tisa ambapo itakuwa mwisho wa ukusanyaji wa kazi za muziki shiriki," ameeleza.

Aidha Mwenyekiti huyo aliendelea kwa kueleza kuwa hakutokuwa na kazi ya muziki itakayoingia kwenye tuzo bila kupitia katika mfumo huo, pia wasanii wote kutoka Tanzania ambao watawasilisha kazi zao inabidi wawe wanachama hai wa Basata kabla ya kuwasilisha kazi hizo.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Basata Kedmon Mapana, aliendelea kusisitiza wasanii kuwasilisha kazi zao kutokana na tuzo hizo kuonesha katika vyombo vya habari kama MTV Base pamoja na BET.