Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ben Pol: Kufanya shoo nje ya nchi siyo ishu, muziki unataka muda

Muktasari:

  • Kauli hiyo Ben aliitoa akimaanisha ili muziki uendelee kufanya vizuri lazima msanii achukue muda wake wote kutengeneza kilicho bora..

Muda huamua hatima ya kila unachofanya kwa kutaka kiwe endelevu au chenye kuishi kati, kauli hiyo anaifafanua mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bernard Paul Nyang’anga maarufu kama Ben Pol wakati akizungumza na Mwananchi.

Kauli hiyo Ben aliitoa akimaanisha ili muziki uendelee kufanya vizuri lazima msanii achukue muda wake wote kutengeneza kilicho bora.

“Lazima msanii achukue muda wa kuitengeneza sanaa yake hivyo anatakiwa akae chini kama yeye na timu yake watengeneze huo wimbo watulie warekebishe,” amsema Ben,

Hata hivyo, ameeleza kuwa ili muziki uwe bora ni lazima kabla haujatoka usikilizwe na watu tofauti watoe maoni yao na ichukue muda kuwa siyo lazima kuwe na upepo wa stori fulani.

“Kabla haujaamua kuutoa wimbo wako lazima uhakikishe unasikilizwa masikioni mwa watu unaowaamini kisha watoe maoni tofauti na ichukue muda na siyo kwa sababu ya upepo fulani kwa muda huo, basi ukatoa wimbo au muziki wako haraka haraka muda ni muhimu sana kufanya wimbo uwe bora,” alisema Ben


Kiki inamsaidiaje katika muziki?

Kumekuwapo na baadhi ya wanamuziki kabla hajatoa wimbo lazima watangulize kiki kwa kigezo cha kuteka watu, lakini kwa upande wake Ben Pol ameweka wazi kuwa siyo shabiki wa kutengeneza kiki ndiyo atoe wimbo na haungi mkono.

“Mimi siyo shabiki wa mambo hayo ya kiki na siungi mkono kwa sababu inafikia muda watu wanasahau hizo stori na muziki wako, kwani tokea dunia iumbwe zimewahi kutokea stori nyingi sana, kwa hiyo hakuna kipya,” anasimulia Ben Pol.


Hakuishia hapo Ben alienda mbali zaidi kwa kuwatolea mfano baadhi ya wasanii wakongwe katika muziki kama Mbaraka Mwishehe na Omari Rajabu akidai kuwa watu wa kizazi hiki hawajui kuwa maisha yao binafsi yalikuwaje, lakini miziki yao bado inaishi.


“Watu hawajui stori za kina Mbaraka Mwishehe, Omari Rajabu kuhusu maisha yao, ndoa zao lakini mpaka leo miziki yao ipo na inaishi. Kwa hiyo kiki sioni kama inaleta mafanikio ya msanii kwenye muziki,” amesema.


Kutofanya matamsha nje ya nchi inamshushaje msanii?

Tambo zimekuwa nyingi ambazo zinadaiwa kuwa kutokufanya matamasha mbalimbali ya njee kwa baadhi ya wasanii inashusha ubora msanii lakini Ben anasema haamini kutofanya show za nje kunaweza kumshusha msanii.


Hivyo ameeleza kuwa kwanza lazima mwanamuziki ajue mashabiki wake anaoenda kuwapa burudani ni wakinanani kwa sababu siyo lazima msanii akafanye show njee ndiyo aonekane kama atakuwa ameshajua watu gani ambao wanapenda burudani yake.


“Siamini kutokufanya sho nje kunaweza kumshusha msanii kwa sababu lazima mwanamuziki ajue ‘audiance’ yake kina nani na je wanataka kitu anachofanya, siyo lazima afanye shoo Japan endapo ameshajua mashabiki wake ni watu wa aina gani wanaopenda anachokifanya,” amesema Ben.


Pia Ben Pol amekazia kuwa kabla ya kufanya show za njee lazima msanii afanye maandalizi ya kwake binafsi kwa ajili ya kwenda kutoa burudani ambapo pia kuangalia hadhira ambao anaenda kuwapa burudani kwa muda huo wanataka nini.


“Kitu cha kwanza ambacho na kifanya kabla ya kwenda kwenye shoo za nje ni maandalizi binafsi hasa katika kufanya mazoezi ya muziki ambao nitaenda kuimba siku hiyo pia msanii anatakiwa kujua mashabiki ni wa zamani au wapya na aendane nao vipi,” anasimulia Ben Pol.


Kwanini ameacha kufanya maigizo?

Mbali na muziki Ben ana kipaji cha kuigiza na aliwahi kuonekana katika tamthilia ya Pazia, japo upande huo amekuwa haonekani mara kwa mara, hivyo ameeleza kuwa hajaacha kufanya maigizo ila kutokana mambo mengi hapo awali ilimbidi asimame kwanza.


“Sijaacha kufanya maigizo kwani nishawahi kufanya tamthilia ya Pazia lakini kutokana na mambo mengi ya ‘ku-shoot’ video za muziki ikanibidi nisitishe kwa muda kidogo ila ni kitu ambacho nakipenda nimekifanya tokea nipo mdogo so naweza nikafanya tena,” anasimulia.