Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bongo ilimtambua Wema Sepetu kabla ya mitandao ya kijamii

Muktasari:

  • Mashindano ya Miss Tanzania kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 1967 na mrembo wa kwanza kutwaa taji hilo alikuwa ni Theresa Shayo, kisha yalisimama hadi mwaka 1994 na mrembo Aina Maeda kunyakua taji hilo.

Dar es Salaam. Katika historia ya shindano la Miss Tanzania, Wema Sepetu ndiye Miss aliyeandikwa na kujadiliwa sana na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii. Mtindo wake wa maisha na kazi vinaruhusu hilo kwa kiasi chake.

Mashindano ya Miss Tanzania kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 1967 na mrembo wa kwanza kutwaa taji hilo alikuwa ni Theresa Shayo, kisha yalisimama hadi mwaka 1994 na mrembo Aina Maeda kunyakua taji hilo.

Baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema alikwenda kushiriki mashindano ya urembo ya dunia (Miss World) kama ilivyo taratibu yaliyofanyika Warsal, nchini Poland.

Matumaini yalikuwa makubwa kwa Wema, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Mtanzania mwenziye, Nancy Sumari kushinda taji la Miss World Africa (Continental Queen of Africa). Lakini Wema alishuhudia taji hilo likienda kwa Stiviandra Oliveira kutoka Angola.

Katika Miss Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo ndiye alishika nafasi ya pili. Huku ya tatu ikienda kwa Lisa Jensen ambaye mwaka 2012 aliteuliwa na kamati ya Miss Tanzania kupitia shindano maalumu (Miss World Second Chance) kushiriki Miss World.

Hiyo ni baada ya ratiba ya mashindano hayo kubadilika na hivyo kuathiri upatikanaji wa kawaida wa Miss Tanzania kwa mwaka huo ambao Brigette Alfred ndiye aliyetwa taji akiwa na umri wa miaka 18.

Baada ya kukabidhi taji la Miss Tanzania, Wema alielekea nchini Malaysia aliposomea Biashara ya Kimataifa (International Business) katika Chuo Kikuu cha Limkokwing. Hata hivyo, hakumaliza masomo yake baada ya kunogewa na uigizaji wa filamu, kitu kilichokuja kumpata umaarufu zaidi.

Wakati yupo Malaysia ndipo filamu yake ya kwanza kucheza ilipotoka, ‘A Point of No Return’ akitumia jina la Dina, akiwa na marehemu Steven Kanumba ambaye ndiye aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa filamu.

Wema na Kanumba waliigiza filamu maarufu kama ‘Family Tears’ (2008), ‘Red Valentine’ (2009) na ‘White Maria’ (2010) ambazo ziliweka jina la mrembo huyo sehemu ya juu kabisa kwenye kada hiyo.

Mwaka 2017 Wema aliachia filamu yake, ‘Heaven Sent’ akiigiza kama mhusika mkuu akishirikiana na Gabo, hii ilifanya vizuri na kuchaguliwa kuwania vipengele saba katika tuzo za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) ambapo alishinda mbili kama mwigizaji bora wa kike na chaguo la watu.

Kwa ujumla Wema ameigiza filamu zaidi ya 25, ameshirikiana na waigizaji wakubwa Bongo kama Jacob Steven (JB), Single Mtambalike, Elizabeth Michael (Lulu), Irene Uwoya, Kajala Masanja, Hemed PhD, Riyama Ally, Aunty Ezekiel, Jacqueline Wolper, Patcho Mwamba, Yusuph Mlela, Gabo na wengineo.

Urembo na filamu vimemfanya Wema kuwa maarufu kabla hata ya mitandao ya kijamii kushika kasi Tanzania na ameendelea kuwa hivyo hadi utawala huu wa Instagram, Snapchat na TikTok.