Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Corona yakatisha shoo za Diamond barani Ulaya

Muktasari:

Kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mataifa mbalimbali barani Ulaya kumekatisha shoo za muziki za msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Dar es Salaam. Kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika mataifa mbalimbali barani Ulaya kumekatisha shoo za muziki za msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Diamond alikuwa na shoo katika nchi mbalimbali barani humo lakini kutokana na baadhi ya nchi hizo kukumbwa na ugonjwa huo, hataweza kufanya shoo yoyote.

Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Nassib Abdul kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameeleza kusitishwa kwa shoo hizo na kwamba zitapangwa tena baadaye.

Kutokana na tishio la kusambaa kwa ugonjwa huo mataifa mengi yamezuia mikusanyiko ya watu.

Mbali na Ubelgiji, Diamond alipanga kufanya shoo Ufaransa, Ujerumani,  Finland na Sweden.