Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye Wema Sepetu ajifungua mtoto wa kiume

Muktasari:

  • Wema Sepetu amebarikiwa kupata mtoto wakiume na mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa Bongofleva Whozu.

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amejifungua mtoto wa kiume akiwa na mchumba wake ambaye ni msanii wa Bongofleva, Oscar John maarufu Whozu, na kuhitimisha safari ndefu ya kusubiri iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wake.

Taarifa za kujifungua kwa staa huyo zilisambaa Ijumaa, Juni 12, 2026, na kuibua furaha mitandaoni, huku mashabiki, marafiki na watu mbalimbali wakituma salamu za pongezi kwa wawili hao.

Kujifungua kwa Wema kumekuja baada ya miaka mingi ya changamoto na simulizi mbalimbali kuhusu safari yake ya kutafuta mtoto, jambo ambalo amewahi kulizungumzia hadharani katika mahojiano na kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa muda mrefu, Wema amekuwa akieleza hamu yake ya kuwa mama huku akikiri kuwa suala la kutopata mtoto lilikuwa miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakimuumiza zaidi maishani mwake.

Mbali na kukabiliwa na presha kutoka kwa jamii, staa huyo pia aliwahi kufichua kuwa alipitia changamoto za kiafya zilizomlazimu kusafiri hadi India kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ovari zake mwaka 2018.

Katika safari hiyo, Wema pia aliwahi kukumbana na maumivu ya kupoteza ujauzito, lakini aliendelea kuwa na matumaini kuwa siku moja angefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuwa mama.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo wa kiume sasa kunafungua ukurasa mpya katika maisha ya Wema na Whozu, huku simulizi yake ikiendelea kugusa wengi waliokuwa wakifuatilia kwa miaka mingi safari yake yenye majaribu mengi kabla ya kufikia furaha hiyo.

Safari ya Wema Sepetu kutoka kuitwa tasa, kufanyiwa upasuaji India, kupoteza ujauzito hadi hatimaye kuwa mama.

Kupitia ukurasa rasmi wa Wema Sepetu ameeleza furaha yake ya kupata mtoto huku Whozu akichapisha maneno haya katika ukurasa wake.

“Sio kuwa tu wazuri sana mbele zake lakini ilimpendeza aonyeshe ukuu wake kwenye uso wa dunia kuwa makadirio ya wanadamu hayawezi kushinda kudra zake.

“Hakika Mwenyezi Mungu amejidhihirisha na kutupa kibali. Hongera shunu wangu na Akhsanteni nyote mliokuwa mkituombea, Mungu yupo na wanaomtumaini Tusichoke kukesha tukiomba maana yeye ni mwenye Huruma siku zote,”ameandika Whozu