Wema Sepetu kuna kitu anaficha?
Muktasari:
Kwa waliomzoea Wema, amekuwa mtu wa mitandaoni kuposti matukio yake mara kwa mara, akihusishwa pia na mahusiano na wasanii mbalimbali na kupenda kujiposti, lakini ukimya huo umewashtua mashabiki wake na kubaki na maswali ya nini kinaendelea.
Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu amezua maswali mitandaoni kutokana na mabadiliko yake ya ghafla ya maisha.
Kwa waliomzoea Wema, amekuwa mtu wa mitandaoni kuposti matukio yake mara kwa mara, akihusishwa pia na mahusiano na wasanii mbalimbali na kupenda kujiposti, lakini ukimya huo umewashtua mashabiki wake na kubaki na maswali ya nini kinaendelea.
Linaloibua maswali zaidi ni posti zake ambazo baadhi amekuwa akiweka picha au video zisizoonyesha mwili wake wote na kuwafanya baadhi ya watu kujiuliza sababu za mabadiliko hayo tofauti na walivyomzoea.
Pia ilisambaa picha inayodaiwa kumwonyesha akiwa anafanya kipimo cha 'ultrasound', huku kwenye picha hiyo ikionekana kama kuna kiumbe tumboni, jambo lililowachanganya baadhi ya watu na kuamini huenda ni ishara ya ujauzito.
Hata hivyo, madai hayo yamegawanyika na baadhi wamekuwa wakisema huenda picha hiyo imetengenezwa au kuhaririwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa (AI), huku wengine wakisisitiza inaweza kuwa ya kweli, lakini hadi sasa Wema hajazungumzia wala kuthibitisha chochote.
Wapo pia waliodai kumwona hivi karibuni na ameonyesha mabadiliko kidogo ya mwili, ikiwemo kuongezeka uzito, jambo linalozidi kuongeza mjadala, ingawa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuhusu kinachoendelea.
Hadi sasa, Wema ameendelea kubaki kimya, jambo linaloacha maswali kwa mashabiki wake na wengi wanasubiri kusikia majibu ya maswali yao kutoka kwake ili kujua ukweli.
Mbali na hilo, muigizaji huyo pia amepunguza kujitokeza kwenye mikusanyiko ya kijamii, tofauti na ilivyozoeleka hapo awali alipokuwa miongoni mwa watu waliojihusisha na matukio mbalimbali.