Jide ni bora chini ya Jangwa la Sahara
Muktasari:
- Nenda Congo, Kenya, South na popote pale kwa mataifa ya SADC. Hutampata mwanamuziki wa kike mwenye muendelezo bora wa muziki zaidi ya Jide. Wakati Mondi anatambua na Komasava, hiki kitu Jide alikifanya miaka kabla Mondi hajabalehe. Alikuwa na pini lililobamba sana la Distance.
Dar es Salaam, Jide ni mwanamuziki bora wa kike chini ya Jangwa la Sahara. Na hii ni kwa miongo miwili iliyopita. Ubora wake ni kwa kila kitu. Albamu nyingi kuliko yeyote wa kike. Ana ‘hits song’ nyingi na zaidi ni amedumu kuliko yeyote.
Nenda Congo, Kenya, South na popote pale kwa mataifa ya SADC. Hutampata mwanamuziki wa kike mwenye muendelezo bora wa muziki zaidi ya Jide. Wakati Mondi anatambua na Komasava, hiki kitu Jide alikifanya miaka kabla Mondi hajabalehe. Alikuwa na pini lililobamba sana la Distance.
Wimbo huo uliimbwa kwa lugha nyingi sana. Na ulitamba karibu Afrika nzima kwa wakati ule, huku baadhi ya wasanii wa mataifa kadhaa wakitamani kuufanyia remix. Pini kali kuanzia audio hadi video kwa nyakati zile. Hali iliyofanya mwanadada ajikombee tuzo kibao.
Nakupenda, nakutaka, nakuhitajiii-iiii...
Moyo wangu wakuwaza, mpenzi uko mbali nami...
Ngiyakuthanda, ngiyakufuna, ngiyakudinga
Nhliziyo yami, ngicabanga ngawe, kodwa ukude nami mpenzi...
I love you, I want you, and I need you
My heart is thinking of you, but you’re far away from me...
Je t’aime, je t’ave, je besoin du toi
Mmh mon coeur te pans, Mh tiele du moi
Nalingiyo, naleliyo, naza naposa nayo
Motema nanga ezokanisa yoo, ozali mosika nanga
Ndagukunda, ndagushaka, ndagukeneye...
Umutima wanje ula kwiyumvila, aliko ulikule chane
Nze nkwagala, nkwagala, nkwagala nyo-oo-oo
Umutima gwange gukulowoza, naye oliwala nyo nange.