Jiongeze: Kanumba aliishi duniani kwa siku elfu 10,317 tu!
Muktasari:
- Ni vyema ukafurahia zaidi kila siku iendayo kwa Mungu. Kwa sababu nafasi ndogo sana ya kufanya vitu vya kuacha ‘legasi’. Mtindo wa maisha huchangia sana kufupi-sha afya na uhai wa washikaji wengi sana. Kama upo salama shukuru Mungu.
Dar es Salaam. Kwa kuhesabu muda kati ya tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kifo. Ni wazi kwamba wanadamu tunaishi kwa siku chache sana duniani. Unaposhindwa kabisa kufurahia maisha ujue wewe ni kilaza ambaye hujui ufupi wa maisha uliyonayo.
Ni vyema ukafurahia zaidi kila siku iendayo kwa Mungu. Kwa sababu nafasi ndogo sana ya kufanya vitu vya kuacha ‘legasi’. Mtindo wa maisha huchangia sana kufupi-sha afya na uhai wa washikaji wengi sana. Kama upo salama shukuru Mungu.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Alizaliwa tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia tarehe 14 Oktoba, 1999. Hii ina maana kwamba Julius aliishi miaka 77 na siku 184, sawa na takribani siku 28,310 tu. Siku efu 28 kwa mtu kama yeye ni chache sana.
Ali Hassan Mwinyi yeye alizaliwa tarehe 8 Mei, 1925. Alifariki dunia tarehe 29 Feb-ruari, 2024. Hii ina maana Mzee Ruksa aliishi miaka 98 na siku 297, sawa na ta-kribani siku 36,091. Pamoja na sifa za kuishi kwake muda mrefu ila ni siku elfu 36 tu.
Benjamin William Mkapa yeye alizaliwa tarehe 12 Novemba, 1938. Na alifariki dunia tarehe 23 Julai, 2020. Hii ina maana aliishi miaka 81 pekee na siku 254, sawa na takribani siku 29,839. Big Ben alimzidi Julius siku kama buku na ushee.
Kwa ujumla marais wote watatu, waliishi siku 94,240, sawa na miaka 257 na siku 5. Huku John Magufuli aliyezaliwa 29 Oktoba, 1959, alifariki dunia tarehe 17 Machi, 2021. Yeye aliishi jumla ya siku 22,421. Sawa na miaka 61, miezi 4 na siku 16.
Staa Steven Kanumba alizaliwa 8 Januari, 1984 na alifariki 7 Aprili, 2012. Kutoka tarehe ya kuzaliwa hadi tarehe ya kifo chake, aliishi kwa jumla siku 10,317. Sawa na miaka 28, miezi 2, siku 30, yaani siku moja kabla ya kutimiza umri wa miaka 28 na miezi 3.