Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jose Chameleone: Mtanzania mwenye asili ya Uganda

Muktasari:

  • Ndani ya studio za Ogopa Deejays, Nairobi, Joseph alifanya kweli na wimbo “Bag-eya”, uliochengua vema Uganda na Kenya. The Kenya’s finest, Redson, alitisha kwenye ngoma hiyo. Mwaka 2001, ikawa mwanzo wa utawala wa Joseph East Afri-ca, alipofyatua hit ya eneo lote la Maziwa Makuu, “Mama Mia”.

Dar es Salaam. Milenia ya tatu ilikuwa inausabahi ulimwengu. Ni mwanzo wa Karne ya 21, hii ni kwa mujibu wa Gregorian Calendar. Mwaka ni 2000, Joseph Kibweteere alishazingua kinoma Uganda, alisababisha vifo vya watu 778. Kipindi hichohicho, Joseph mwingine alikuwa Kenya akitengeneza heshima ya Uganda.


Ndani ya studio za Ogopa Deejays, Nairobi, Joseph alifanya kweli na wimbo “Bag-eya”, uliochengua vema Uganda na Kenya. The Kenya’s finest, Redson, alitisha kwenye ngoma hiyo. Mwaka 2001, ikawa mwanzo wa utawala wa Joseph East Afri-ca, alipofyatua hit ya eneo lote la Maziwa Makuu, “Mama Mia”.
Joseph huyu hakuwa Kibweteere. Ni Joseph Mayanja. Business moniker ni Chame-leone. Tamka, Jose Chameleone, kisha tembea na jina hilo Afrika Mashariki yote, ushuhudie ukuu wake ulivyotamalaki nchi kwa nchi.



 Baada ya Mama Mia kuhodhi airwaves za Afrika Mashariki, Chameleone aliamua kujiundia tabia ya kuteremsha hit baada ya hit. Kila kazi aliyoachia, iligeuka dude la East Africa. “Njoo Karibu”, “Jamila”, “Sauti ya Dhahabu”, “Mambo Bado”, “Kipepeo”, “Bahati Yangu”, “Shida za Dunia”. Hatujamaliza.


 Kabla ya kuendelea kushusha vyuma, tukumbuke songombingo la Joseph wawili, Mayanja na Haule ambaye dunia inamwita Profesa Jay. Mdundo wa ngoma “Niku-saidieje” wa Profesa Jay, Chameleone akautumia kutoa kitu, “Bomboclaat”. Kisha, Joseph wawili wakaingia studio wakafyatua anthem, “Ndivyo Sivyo”. Amani ika-tawala. Mgogoro wa kazi ukasuluhishwa kwa kazi.


Tuendelee sasa; “Bei Kali”, “Mama Rhoda” ft Bushoke, “Dorotia”, “Vumilia”, “Naom-ba Uniamini”, “Naumia”, “Badilisha”, “Valuvalu”, “Tubonge”. Zote hizi ni East African hits. Ni kwa sababu hiyo, Chameleone akiwa Kenya, kama yupo Uganda, anapokuwa Tanzania, anasahau kama alizaliwa Kampala.


 Ukuu wa Chameleone unajengwa na uandishi wake. Kutoka wimbo hadi wimbo, husimulia hadithi yenye mafunzo. Ametengeneza sound yake ya kipekee. Huwezi kuinakili wala kuiiba. He is the very best of East Africa.


 Chameleone ni mzawa wa Uganda. Luganda ndiyo lugha yake namba moja, halafu Kiingereza kinafuata. Zipo nyimbo ameimba Luganda na Kiingereza, lakini mapema kabisa aliamua kujifunza Kiswahili ili kukitumia kuufikisha muziki wake mbali. Mwa-limu wake wa Kiswahili Redson.



 Kutoka “Mama Mia” mpaka “Tubonge”, “Jamila” hadi “Valuvalu”, Chameleone amekivaa Kiswahili kama beji ya heshima. Tanzania ndiyo makao makuu ya Kiswahili duniani. Kitendo cha Chameleone kutumia Kiswahili, kimekuwa kikiwafanya Watan-zania wamwone ni Mswahili mwenzao. ‘Now you’ kwa nini Chameleone ni jina lenye nguvu kwenye ardhi ya Mwalimu Nyerere.


 Nyimbo za Chameleone hubeba ujumbe halisi wa maisha ya Afrika Mashariki. Anza na “Mama Mia”, mbona simulizi za wanaume kuachwa ni nyingi Kenya mpaka Tan-zania? Akina “Jamila” na hadithi zao za kushobokea ving’aavyo kwa pupa wakidhani dhahabu, baadaye wanagundua shaba na kutaka kurejea kwa waliowatosa mwan-zoni, ni mambo ya kila siku DRC mpaka Rwanda.


 Naweza kukumbuka mwaka 2006 wakati “Bahati Yangu” inatoka. Uliimbwa Bongo utadhani wimbo wa kizalendo wa “Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.” Ujumbe wake ulikuwa unachoma Mbagala, Dar es Salaam, mpaka Nangurukuru, Lindi.


 Vijicho pembe wapo duniani kote. Mtu anakuletea fitina kisa anaona mambo yako yanakunyookea. Chameleone akaimba “Fitina yako bahati yangu, aliyepanga changu ni changu.” That’s gangster, kama wasemavyo Wamarekani Weusi. Mungu ndiye mpangaji wa kila kitu. Sasa kaamua mwenzako apate hicho alichonacho. Wewe unavimba mashavu na kutengeneza fitina.


 “Shida za Dunia” inaliwaza kuanzia Chunya mpaka Nyarugusu. Ukweli ni mmoja tu, muziki wa Chameleone unagusa maisha ya kila siku ya Mbantu. Tungo zake hugusa nyoyo kwa ndani kabisa. Chameleone siyo mwanamuziki wa majoka, mapanga na kwata. Ni mwanamuziki wa tenzi za kwenye mtima.
 Msanii bora anayeishi na kufikia daraja la kuitwa legend, lazima atakuwa na silaha inayomtofautisha na wengine. Nguvu ya sauti ya Chameleone hakuna namna una-weza kuifananisha na yeyote. Uimbaji wa Chameleone unakupa picha ya ujazo wa nishati alionao.


 Tunaweza kupingiana kama umezichoka pesa zako. Mtaje mwanamuziki Afrika Mashariki anayegonga high note kumzidi Chameleone Kusini ya Jangwa la Sahara. Uone pesa yako itakavyohamia kwangu kiulaini. Jumlisha hili; sauti ya Chameleone ina mkwaruzo fulani, kitu ambacho kinaongeza ladha ya nyimbo zake, kuzifanya zipenye utamu masikioni.


 Chameleone ni jina ambalo limeinakshi Bongo Fleva. Nyakati za mwanzo za utawala wa Bongo Fleva kwenye mainstream media Tanzania, Chameleone alikuwapo na uhusika wake wake ulikuwa dhahiri. Nyimbo za Chameleone zilipigwa sanjari na za wanamuziki wa Tanzania. Chameleone alitamba kwenye chati za Bongo Fleva.


Mchango wa nyimbo za Chameleone kwenye Bongo Fleva, ulisababisha maudhui ya Bongo Fleva yapate nguvu zaidi. Hii haikumfanya Chameleone kutambulika kuwa mi-ongoni mwa wanamuziki wa Bongo Fleva peke yake, bali pia ilimwezesha kuvuna mamilioni ya mashabiki pembe zote za Tanzania.


 Ungemwona Chameleone miongoni wanamuziki wa Kitanzania, kama mapacha. Un-aweza vipi kusahau upacha wa Chameleone na Mfalme wa Takeu, Mr Nice? Hata tukio lenye kukumbukwa kwa ubaya mno katika muziki wa Bongo Flava, Dudubaya kumvamia Mr Nice na kumshambulia jukwaani, Chameleone alikuwepo.



 Yes, ilikuwa mwaka 2004. Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga. Mr Nice akiwa na Chameleone jukwaani, Dudubaya alitenda tukio haramu, ambalo lililaaniwa na kila mdau wa muziki. Alimvamia Mr Nice na kumporomoshea kisago. Hatufukui maka-buri babu, tunashusha facts za upacha wa Chameleone na Bongo Fleva.


Je, tukumbushe tukio la Chameleone kuanguka ghorofani Arusha ndiyo ukubali ku-wa amefanya ziara maeneo mengi Tanzania, kuliko msanii mwingine yeyote wa Af-rika Mashariki wa kutoka nje ya Bongo? Hata Chameleone mwenyewe anatambua kuwa muziki wake usingebeba uzani ambao unao kama usingekumbatiwa na Wabongo.


Bongo Fleva Honors ni jukwaa la utunzaji wa historia na utamaduni wa Bongo Fleva. Muhimu zaidi, huwatambulisha na kuwatunuku hadhi wanamuziki wa Bongo Fleva wenye mchango mkubwa katika ukuaji wa muziki huo, na ambao wameweza kuufanya muziki huo kuwa utamaduni wenye nguvu Afrika. Tangu Januari 2023, Bongo Flava Honors imekuwa ikiwatambua wana-Bongo Fleva wa Tanzania.


 Julai 31, 2026, The Super Dome, Oysterbay, Bongo Flava Honors itamtunuku Cha-meleone hadhi ya hall of fame. Akiwa wa kwanza kutoka nje ya Tanzania. Utapigwa muziki wenye uzani wa kuufungua Mlango Bahari wa Hormuz. Sugu the Jongwe atasimamia show yote, hatua kwa hatua, kuhakikisha heshima ya Chameleone kwenye Bongo Fleva inaenziwa ipasavyo.