Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala hataki tena mapenzi ya mtandaoni

Muktasari:

  • Mwananchi limetonywa, Kajala amewekewa ulinzi huo na mumewe huyo mtarajiwa ambaye amekuwa akifichwa jina lake huku akipigwa biti kuachana na kiki zinazohusu mapenzi kwani zinamshushia hadhi hiyo jamaa yake.

Dar es Salaam. Kama uliwahi kumkatia tamaa msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja kwa kudai umri umeenda na hatoweza kuolewa,  basi imekula kwako, kwani tayari ameshavalishwa pete ya uchumba na kuwekewa ulinzi mkali kila aendapo.

Mwananchi limetonywa, Kajala amewekewa ulinzi huo na mchumba wake huyo mtarajiwa ambaye amekuwa akifichwa jina lake huku akipigwa biti kuachana na kiki zinazohusu mapenzi kwani zinamshushia hadhi hiyo jamaa yake.

“Habari ya sasa mjini ni  Kajala amepata Pedeshee na tayari ameshavishwa pete ya uchumba na baada ya kuvalishwa amewekewa ulinzi binafsi, hivyo kila anapokuwa lazima awe na bodigadi.”

Mwananchi lilimtafuta Kajala ili kuthibitisha habari njema hizi na alisema  maneno machache tu, wakati wa Mungu ni sahihi na kufanya mambo kimya kimya ni vema zaidi kwake.

“Waoooh hizi habari unazonipa  ni jambo la kheri kwangu, lakini niseme tu kwa sasa mambo yangu ya mahusiano siwezi kuyaweka wazi.

"Basi kama suala hilo lipo basi vyema zaidi kwangu. Kuhusu kuonekana na pete mkononi ni jambo la kawaida kwa mwanamke na hata ishi ya kuwa na walinzi sehemu tofauti tofauti napokuwa pia ni kawaida ni kwa ajili ya usalama zaidi” alisema Kajala.