Kanye West abadili jina, ataka aitwe YE

Muktasari:

  • Mwaka 2021, jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la kubadili jina la kisheria la YE. West amefanya maamuzi hayo kutokana na albamu yake ya nane kubeba jina hilo na tayari anatumia akaunti hiyo ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni 19.

Marekani. Rapa kutoka Chicago nchini Marekani Kanye West, inaonekana amechoshwa na watu kutumia jina lake la zamani na badala yake kuwataka watumie jina jipya la kisheria.

"Ninafunga akaunti yangu ya Instagram ya Kanye West. Jina langu ni Ye. Hakuna chapa itakayonilazimisha kuitwa kile wanachotaka mimi niendelee kuitwa,” amesema West alipokuwa akizungumza na mtangazaji wa chaneli ya Revolt Justin Laboy, Februari 28, 2024.

Hata hivyo, West hawezi kupata ukurasa mpya kwenye mtandao huo kwa sababu tayari kuna mtu anatumia jina la YE.

 "Kuna mtu ana akaunti anayotumia jina ninalotaka kulitumia, ningependa kuwa na hilo jina langu la kisheria. Hakuna mtu atakayenitisha, sasa ukiniita Kanye West, basi unanitoa kwenye jina langu." 

Baadaye Laboy alimtumia ujumbe YE kwamba Instagram imeridhia suala la kumpatia akaunti itakayokuwa na jina analolihitaji yeye, huku akinukuu maneno ya mwakilishi wa mtandao huo wa Instagram "Watendaji walikuwa ofisini na walipiga simu mara moja, Ninangoja taarifa wanazohitaji ili kufanya iwezekane leo."

Mwaka 2021, jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la kubadili jina la kisheria la YE. West amefanya maamuzi hayo kutokana na albamu yake ya nane kubeba jina hilo na tayari anatumia akaunti hiyo ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni 19.