Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kim Kardashian adai kuzoea kuwa single!

Muktasari:

  • Ni takribani miaka mitano tangu Kim alipotalikiana na aliyekuwa mume wake, rapa Kanye West, 48, na tangu wakati huo hajaonekana hadharani akiwa na mwanaume mwingine, jambo linalowatatiza mashabiki wake.

Marekani. Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu Marekani, Kim Kardashian, 45, amefunguka kuhusu maisha yake ya kimapenzi kwa sasa akieleza sababu za kutokuwa na uhusiano mpya licha ya shinikizo analopata.

Ni takribani miaka mitano tangu Kim alipotalikiana na aliyekuwa mume wake, rapa Kanye West, 48, na tangu wakati huo hajaonekana hadharani akiwa na mwanaume mwingine, jambo linalowatatiza mashabiki wake.

Akizungumza katika kipindi kipya cha Keeping Up With The Kardashians kilichorushwa hivi karibuni kupitia Hulu, Kim alidai kuwa muda mrefu aliotumia akiwa single umemfanya kuzoea hali hiyo!

Mwanzilisha huyo wa chapa ya mavazi ya Skims, alifafanua kwamba kadiri muda unavyosonga, wazo la kushiriki maisha yake ya ndani na mtu mwingine ndivyo linazidi kukosa mvuto kwa upande wake.

“Unapokaa muda mrefu ukiwa single, unazidi kuzoea, na mawazo ya kuwa na mtu wa karibu yanapungua na hata kukosa mvuto,” alisema Kim katika mahojiano hayo yaliyolenga kuibua mambo ya ndani zaidi.  

Kauli yake ilikuja baada ya mwigizaji Sarah Paulson ambaye wamecheza pamoja tamthilia ya All’s Fair (2025), kumtaka Kim kuwa na ‘baby mpya’ na kuacha kujilinda kupita kiasi.

Sarah alidai amekuwa akiona jinsi Kim anavyojitahidi kulinda maisha ya watoto wake, North (12), Saint (9), Chicago (7) na Psalm (5), hali inayoweza kumzuia kufungua moyo wake katika uhusiano mpya.

Kim alikiri kuwa amejiwekea mipaka linapokuja suala la uhusiano mpya tangu kutoka kwa talaka yake, na kwa sasa kipaumbele chake ni kazi na familia kuliko kutafuta penzi jipya. Hata hivyo, alibainisha kuwa hajafunga kabisa mlango huo.

“Unajua mimi ni mtu wa kuamini sana kwenye mapenzi. Mtu sahihi akija, nitakuwa tayari na kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Kim, mrembo mwenye utajiri wa Dola1.7 bilioni, wastani wa Sh4.1 trilioni.

Ikumbukwe uhusiano wa Kim na rapa Kanye West (Ye) ulianza Aprili 2012. Walifunga ndoa Mei 2014 huko Florence, Italia, ambapo harusi yao ilikuwa ya faragha kiasi kwamba hakuna aliyeruhusiwa kupiga picha.

Hata hiyo, baada ya miaka sita ya ndoa wakiwa tayari wamejaliwa watoto wanne, Kim aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani hapo Februari 2021. Mchakato wa talaka yao ulikamilika rasmi Novemba 2022.

Kabla ya Kanye West kuwa na Kim, alishakuwa na uhusiano na warembo kadhaa, miongoni mwao ni Alexis Phifer (2000 - 2006), Amber Rose (2008 - 2010), Julia Fox (2021) na Venetria (2022).

Lakini uhusiano wake na Kim ndio uliyodumu kwa muda mrefu zaidi takribani miaka 10, na hadi sasa ndio uhusiano pekee uliompatia watoto rapa huyo aliyevuma zaidi kupitia albamu, The College Dropout (2004).