Kompa fleva yang'ara kiwanda cha muziki bongo 2024
Muziki wenye miondoko ya taratibu maarufu kama Kompa Fleva umeripotiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye kiwanda cha Bongo Fleva kwa kuiteka jamii ya Watanzania kutokana na muundo wake wa kipekee.
Mtandao wa ‘Audiomack Africa’ umeweka wazi kuwa muundo wa muziki huo ni wa kipekee zaidi hasa ukichanganywa na melodi zenye maneno ya Kiswahili.
“Kwa kuchanganya melodi za Kiswahili na midundo ya jadi ya ngoma za Haiti pamoja na solo za synth, Kompa Fleva imekuwa sauti ya pekee ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2024,” taarifa ya Audiomack Africa imebainisha hivyo.
Mbali na kutoa taarifa hiyo, lakini pia zipo ngoma ambazo zimepelekea muziki huo kutamba zaidi ikiwemo Zawadi na Pwita kutoka kwa msanii Zuchu, Far Away ya Genius Jini ft Jay Melody, Usemi Sina ya Nandy ft Harmonzie, Mchuchu ya Mocco ft Alikiba, Nisiulizwe ya Jux na nyinginezo.
Kompa Fleva ni aina ya muziki wa taratibu wenye ladha ya kipeee ambao asili yake ni Comoro na Haiti.