Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwaito ilikuwa habari ya mjini kabla ya Amapiano

Muktasari:

  • Kwaito Dance ni mtindo wa kucheza uliyoanzishwa Afrika Kusini, mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kipindi ambacho vijana wengi walikuwa wakipambana kutoka kwenye mfumo wa ubaguzi wa rangi ambapo vijana kutoka katika mitaa ya Soweto, Alexandra na Tembisa walitaka kuanzisha kitu cha kuwatambulisha kama kizazi kipya chenye uhuru na ubunifu

Dar es Salaam. Ukiachana na mambo ya sasa watu kuvutiwa na muziki wa ‘Amapiano’. Hapo awali kulikuwa na ‘Kwaito’ aina ya muziki ambao ulipelekea kuanzishwa kwa staili ya uchezaji ijulikanayo kama ‘Kwaito Dance’.

Kwaito Dance ni mtindo wa kucheza uliyoanzishwa Afrika Kusini, mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kipindi ambacho vijana wengi walikuwa wakipambana kutoka kwenye mfumo wa ubaguzi wa rangi ambapo vijana kutoka katika mitaa ya Soweto, Alexandra na Tembisa walitaka kuanzisha kitu cha kuwatambulisha kama kizazi kipya chenye uhuru na ubunifu.

Vijana hao walijikusanya na kuanzisha staili hiyo, ambapo jina linalotajwa zaidi kama mzizi na mwanzilishi wa Kwaito ni Arthur Mafokate ‘King of Kwaito’. Kupitia wimbo wake maarufu wa ‘Kaffir’ alioachia miaka ya 90 ulichochea zaidi muziki wa Kwaito na kuifanya dansi yake kukubalika pande zote za dunia.

Aidha, waanzilishi wa muziki huo walitumia mchanganyiko mbalimbali ili kutengeneza ‘Kwaito’. Ambapo walitumia midundo ya kitamaduni ya Afrika pamoja na rap ya kienyeji, tofauti na nyimbo nyingine. Kwaito ulikuwa muziki wa polepole na beat nzito huku ikiongezewa maneno ya mitaani yaliyogusa maisha ya watu, ukosefu wa ajira, umoja pamoja na matarajio ya vijana.

Mwanzilishi wa muziki wa 'Kwaito' na 'Kwaito Dance' Arthur Mafokate

Ingawa Kwaito Dance bado inapigwa kwenye sherehe mbalimbali lakini umaarufu wake umeshuka huku sababu zikitajwa ni kutokana na mapinduzi katika tasnia ya muziki duniani pamoja na mwenendo wa maisha ya sasa.

Aidha katika makala mbalimbali zinaeleza kuwa moja ya sababu kubwa ya kupotea kwa muziki na dansi hiyo ni kutokana na muziki wa Amapiano kuchukua nafasi kubwa Afrika Kusini. Ambapo mashabiki wengi wa sasa wamejikita zaidi katika muziki huo, huku Kwaito ikipewa kisogo. 

Mbali na hayo imeelezwa sababu nyingine ni mastaa waliokuwa wakitamba kwenye Kwaito kama Arthur Mafokate, Mandoza, TKZee na Boom Shaka, wengi wakipotea kwenye gemu huku wengine wakifariki.

Enzi za uhai wa Kwaito ziliibuka ngoma mbalimbali ambazo zilitikisa mitaa ya Kwamadiba ikiwamo “Nkalakatha” ya Mandoza, “Shibobo” ya TKZee ft. Benni McCarthy, “Kaffir” ya Arthur Mafokate, “Thathi Sgubhu” ya Boom Shaka, “Guz 2001” ya Trompies, “Dlala Mapantsula” ya Mapantsula, “Sista Betina” ya Mgarimbe, “Via Orlando” ya DJ Vetkuk & Mahoota, “Kwenza Kanjani” ya Brown Dash, na “Mshini Wam” ya Big Nuz.