Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maandalizi tamasha la Kizimkazi 2026, yapamba moto

Muktasari:

  • Katika tamasha hilo ambalo limejizoelea umaarufu, kutakuwa maonyesho, burudani na programu mbalimbali za kuvutia zinazolenga kutangaza utalii. Uwekezaji na utamaduni wa Kizimkazi.

Zanzibar. Kizimkazi Kumenoga! Hiyo ndio kauli mbiu iliyobeba Tamasha la Kizimkazi 2026 linalotarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 12 hadi 14,2026 likiwa limesheheni fursa lukuki .

Katika tamasha hilo ambalo limejizoelea umaarufu, kutakuwa maonyesho, burudani na programu mbalimbali za kuvutia zinazolenga kutangaza utalii. Uwekezaji na utamaduni wa Kizimkazi.

Akizungumza leo Julai 8,2026 kuhusu maandalizi ya kuelekea tamasha hilo Wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar, Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Kizimkazi Mahfodh Said Omar amesema katika tamasha hilo miradi mbalimbali ya maendeleo itazinduliwa.

Amesema uzinduzi wa tamasha hilo utafunguliwa rasmi na Rais Zanzibar Dk Ali Hussein Mwinyi na kisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni katika siku ya kufunga tamasha hilo.


“Tunawaalika wawekezaji, wadau wa mandeleo, wafanyabiashara, wadau wa utalii na wananchi kwa ujumla kushiriki Kizimkazi Festival 2026. Kwani mwaka huu tamasha limenoga na limebeba fursa nyingi kwa wote.

“Leo tunazindua rasmi maandalizi ya Kizimkazi Festival 2026. Tamasha hili lilianzishwa na wazee pamoja na wananchi wa Kizimkazi kwa lengo la kuhifadhi na kuenzi utamaduni, mila na desturi za eneo letu. Kadiri miaka ilivyopita, tamasha limeendelea kukua na sasa limekuwa jukwaa muhimu la kutangaza utalii,uwekezaji na mendeleo ya jamii,"amesema

Ameongeza kuwa Kizimkazi Festival ni tamasha la wananchi wa Kizimkazi. Dhamira yake ni kuitangaza Kizimkazi kama eneo lenye historia, utamaduni, vivutio vya utalii na fursa nyingi za uwekezaji kwa manufaa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla.

Kuhusu malengo ya Tamasha hilo amesema ni kutangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya utalii pamoja na kuhifadhi, kuenzi utamaduni wa Kizimkazi.

Akizungumzia miradi itakayozinduliwa wakati wa tamasha hilo ni mradi wa maji Kizimkazi, kiwanja cha watoto Kibu Teni,nyumba za kuishi Bopar Enterprises, Jiwe la msingi Salaam Cane Restaurant-K/Dimbani.

Miradi mingine itakayozinduliwa ni mradi wa mabweni mapya Hasnu Makame Sekondari-Kibuteni ,jiwe la msingi jengo la maendeleo Kibuteni na uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Johari-K Mkunguni.

“Tunawakaribisha wawekezaji, wadau wa utalii, tour operators, tour guides, travel agencies, wadhamini, vyombo vya habari, wasanii, watu mashuhuri na wadau wa maendeleo kushiriki Kizimkazi Festival ili kujionea fursa na kushiriki kuitangaza Kizimkazi duniani.”

Mwenyekiti huyo amesema ujumbe mkuu katika tamasha hilo ni jukwaa la maendeleo linalounganisha utamaduni, utalii na uwekezaji kwa manufaa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Karibuni Kizimkazi Festival mshuhudie utajiri wa utamaduni wetu, mjionee fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii na muwe sehemu ya safari ya kuijenga Kizimkazi kuwa kitovu cha maendeleo,”amesema