Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maisha ya Uche Montana, mwigizaji wa Nigeria anayesumbua 

Muktasari:

  • Hata hivyo kwa mwigizaji wa Nigeria Uche Montana, imekuwa tofauti kwani uthubutu, nidhamu na juhudi zimemfanya kuingia kwenye orodha ya waigizaji wanaokubalika zaidi katika tasnia ya filamu Barani Afrika.

Nigeria. Katika ulimwengu wa burudani, si kila anayeanza safari ya sanaa hufanikiwa kufika kileleni. Wengi huanza kwa ndoto kubwa lakini hukwama njiani kutokana na changamoto mbalimbali. 

Hata hivyo kwa mwigizaji wa Nigeria Uche Montana, imekuwa tofauti kwani uthubutu, nidhamu na juhudi zimemfanya kuingia kwenye orodha ya waigizaji wanaokubalika zaidi katika tasnia ya filamu Barani Afrika.

Uche Montana, ambaye jina lake halisi ni Uche Nwaefuna, alizaliwa Aprili 8, 1994 nchini Nigeria. Amesoma katika Chuo Kikuu cha Lagos akisomea Business Administration. 

Ingawa alijikita upande huo wa biashara lakini mapenzi yake kwenye sanaa ndiyo yaliyomvuta zaidi na hatimaye kuamua kuingia kwenye tasnia ya Nollywood.

Baada ya kuwa na ndoto ya kuingia katika tasnia hiyo tangu akiwa mdogo. Ndoto hiyo ilianza kutimia taratibu ambapo safari yake ya uigizaji ilianza rasmi mwaka 2016 alipopata nafasi katika tamthilia maarufu iitwayo Hush. 

Hii ilikuwa hatua muhimu iliyofungua milango ya mafanikio yake. Kupitia kazi hiyo aliweza kuonesha uwezo wake mkubwa wa kuigiza na kuvutia macho ya wadau wa tasnia ya Nollywood.

Baada ya hapo, alianza kuonekana kwenye filamu na tamthilia mbalimbali, akijizolea umaarufu hatua kwa hatua. Umahiri wake katika kuvaa uhusika kwenye drama za maisha halisi ulimfanya kupendwa zaidi na mashabiki hasa wa kizazi cha sasa kinachopendelea maudhui ya mapenzi (mahusiano).

Aidha ukuaji wa teknolojia na mabadiliko ya namna ya usambazaji wa filamu umemfungulia zaidi milango. Ambapo mwaka 2024 alifungua chaneli yake ya YouTube ‘Uche Montana TV’, kupitia jukwaa hilo alifanikiwa kuwafikia mashabiki wake katika pande mbalimbali za dunia. Mpaka kufikia sasa chaneli hiyo inazaidi ya wafuatiliaji 1.35 milioni.

Hata hivyo moja ya filamu ambayo inafuatiliwa zaidi kwasasa na kutazamwa mara nyingi ni ‘Monica, A True Life Story’ iliyotazamwa mara 12 milioni ikiwa ni wiki mbili tuu tangu kuachiwa kwake.

Mwanzoni, safari hiyo haikuwa rahisi. Ushindani ulikuwa mkubwa, lakini alizingatia mambo ubora wa hadithi, mwendelezo wa utoaji wa maudhui yanayoendana na maisha halisi. Pamoja na kushirikiana na waigizaji wengine maarufu.

Hatua hizo zilifanya chaneli yake kuanza kuvutia watazamaji wengi na hatimaye kujikusanyia mamilioni ya mashabiki duniani .

Katika upande wa uandishi wa stori, Uche Montana hafanyi kazi peke yake. Kama ilivyo kwa wasanii wengi wa Nollywood, hushirikiana na waandishi mbalimbali wa script kulingana na mradi husika. Jambo ambalo humwezesha kupata mitazamo tofauti ya ubunifu na kuleta utofauti katika kazi zake.

Aidha, ingawa si mwandishi mkuu wa kazi zake zote, hushiriki katika kuchagua na kuboresha stori ili ziendane na hadhira yake.


Kuhusu Mahusiano

Licha ya mafanikio yake, Uche Montana ameendelea kuwa msanii anayelinda sana maisha yake binafsi. Tofauti na baadhi ya mastaa wanaoweka wazi mahusiano yao, yeye amechagua kuyaweka faragha, hali inayoongeza mvuto na kuibua maswali miongoni mwa mashabiki wake.

Aidha zipo tetesi kuwa maisha yake yanaendeshwa na sponsa. Lakini wakati alipokuwa akizungumza na mashabiki zake alikanusha suala hilo alieleza kuwa maisha mazuri na kuishi kwakwe kifahari kunatokana na kufanya kazi kwa bidii.

“Kumekuwa na dhana nyingi potofu watu wakiuliza napataje pesa wapenzi wangu, tupo katika kipindi ambacho unaweza kutengeneza pesa kupitia tasnia hii. Na ninajivunia kusema mimi ni mmoja wa watu wanaopata kipato kupitia tasnia hii, na napenda kujifurahisha.

“Nafanya kazi kwa bidii, na pia najifurahisha. Kwa kweli, nafanya kazi zaidi kuliko ninavyojifurahisha. Lakini kuna uwiano, kwa sababu mwisho wa siku mimi ni msichana mdogo nahitaji pia kuunda kumbukumbu maishani. Ni muhimu sana kuunda kumbukumbu ambazo siku moja nitawaambia watoto wangu, nilifanya hiki na kile wakati fulani,”alisema Uche 

Mpaka kufikia sasa ameshaachia filamu mbalimbali katika chanel yake ikiwemo A Place With You (2026), Nine Months Till Forever, Hustle Code, Chaos to Calm, A Lady and Her Gentleman, Love Pursuit, Six Months of Grace, Baby Blues na nyinginezo. Huku mashabiki wakisubiri kwa hamu mwendelezo wa filamu ya Monica inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.