Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maoni ya mashabiki Jux kuibukia kwenye uigizaji

Muktasari:

  • Siku chache zilizopita katika mitandao ya kijamii kumesambaa video zikimuonesha Jux akiwa na mke wake Priscy wakiwa wanaigiza pamoja filamu ambayo inaoneshwa katika mtandao wa YouTube iitwayo ‘ROBO SHAGGI 2’.

Baada ya miaka kadhaa ya kutamba kwenye muziki wa Bongo Fleva na kujiimarisha kama mmoja wa wasanii wenye mvuto mkubwa Afrika Mashariki, msanii Juma Jux ameanza safari mpya katika tasnia ya uigizaji. Hatua ambayo imeibua taswira mpya na maoni mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita katika mitandao ya kijamii kumesambaa video zikimuonesha Jux akiwa na mke wake Priscy wakiwa wanaigiza pamoja filamu ambayo inaoneshwa katika mtandao wa YouTube iitwayo ‘ROBO SHAGGI 2’. Ambapo baada ya video hiyo kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakimponda Jux kuukimbia muziki kutokana na mashabiki kugoma kumsapoti.

Ikumbukwe kwa takribani miezi mitatu imepita kumekuwa na mvutano pamoja na mijadala baina ya mashabiki na wasanii wa Bongo Fleva ambapo baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii walitangaza kutowasapoti wasanii katika kazi zao.

Hata hivyo, hali imekuwa tofauti kwani katika jukwaa la YouTube nyimbo mbalimbali za wasanii zimeendelea kusumbua katika chati hiyo.

Aidha kwa upande wa Jux kuingia katika uigizaji mashabiki wametoa maoni ya kumponda wakidai kuwa muziki umeshamshinda huku baadhi wakimpongeza kwa hatua hiyo.

“Blaza anapiga vimeo vya lamata wa Naija,”, “Huyu jamaa na mke wake wanajua kweli jinsi ya kutengeneza pesa. Mashabiki wake watazidi kuongezeka Nigeria / Afrika Magharibi, na kwa ufupi duniani kote. Hii ndiyo maana halisi ya utafutaji wa kweli kabisa 🔥🔥🔥 Hata kina 50 Cent, DJ Khaled, Chris Brown na T.I wenyewe wanaigiza 🙌 @its.priscy mwanamke shupavu,”

“Duh haki ya Mungu Watanzania kazieni apo apo kuna wasanii watageuka mambondia mmoja uyo kashakuwa Selengo,” , “Watu, hii inaitwa collaboration. Bro Shaggy alimsaidia Jux wakati wa show yake. Jux anachofanya ni kurudisha fadhila, na hivyo ndivyo tunavyokua.

Hata Davido na wasanii wengine wakubwa huwa wanawaunga mkono skit makers na hata streamers, ili pale wanapotoa muziki wao nao wawaunge mkono. Ninyi nyote ni ma-hater; ndiyo maana muziki wa Tanzania haujulikani sana duniani, kwa sababu hamna utamaduni wa kuunga mkono kila mmoja,”

Aidha wengine wameandika; “Waliosema tufanye kazi wanafanya wao kazi wahenga hawaamini macho yao, Bora aendelee kuimba tu, mimi sioni kama Jux ana muonekano wa kuigiza."   "Kweli maisha yameanza kuwapiga wasanii hadi wanaamuza kuingia kwenye uigizaji si mchezo. Hii ndio ile kila mtu atachanganyikiwa kwa wakati wake lakini hongera kwake amejitahidi,” wameandika baadhi ya mashabiki katika mitandao ya kijamii.