Marc Anthony aongeza mtoto wa nane
Muktasari:
- Mnamo Januari, Marc Anthony alitangaza kuwa anatarajia mtoto wa pili katika ndoa yake na aliwahi kuwa Miss Universe Paraguay, Nadia Ferreira, 26, ambaye wamekuwa pamoja tangu mwaka 2023.
Marekani. Mwanamuziki maarufu wa RnB na Pop kutokea Marekani, Marc Anthony, 57, amejaliwa kupata mtoto wake wa nane baada ya kufunga ndoa nne katika maisha yake ikiwamo ile na mwimbaji mwenzake, Jennifer Lopez (J.Lo).
Mnamo Januari, Marc Anthony alitangaza kuwa anatarajia mtoto wa pili katika ndoa yake na aliwahi kuwa Miss Universe Paraguay, Nadia Ferreira, 26, ambaye wamekuwa pamoja tangu mwaka 2023.
Akitangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo wiki hii kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marc Anthony alisema ni furaha katika nyumba yao baada kupata mtoto wa kike ambaye wamempa jina la Myla.
“Ni baraka kubwa sana kuweza kuwataarifu kuhusu kuzaliwa kwa mrembo wetu Myla. Hamuwezi kufikiria furaha tuliyonayo nyumbani kwetu kwa sasa; tupo juu ya mawingu kwa furaha!” aliandika Marc Anthony.
Ikumbukwe mwanamuziki huyo alitangaza ujauzito wa mkewe wakati wakihad-himisha miaka mitatu ya ndoa yao iliyofungwa Januari 28, 2023 huko Florida, Ma-rekani.
“Heri ya kumbukizi ya miaka mitatu ya ndoa, ni zawadi kubwa sana ambayo maisha imetupa. Mungu ni mkuu, mtoto wetu Marquito anaenda kuwa kaka mkubwa,” aliele-za.
Marc Anthony, mkali wa kibao, You Sang To Me (1999), mtoto wake wa kwanza na Nadia, Marquito alizaliwa Juni 2023, miezi michache baada ya wao kufunga ndoa.
Tetesi za wawili hao kuwa pamoja zilianza kufuatia matembezi yao huko Mexico City mnamo Machi 2022 na walithibitisha uhusiano wao kupitia Instagram kwa kuposti picha ya selfie waliyopigwa kwenye ndege.
Hatimaye walitangaza kuchumbiana mnano Mei 2022 wakati wa sherehe katika mgahawa wa Sexy Fish huko Florida, huku Nadia akionyesha picha ya pete ya al-masi aliyovishwa kwenye Insta Story yake.
Wawili hao walifunga ndoa Januari 28, 2023 kwenye jumba la makumbusho la Pe-rez huku mastaa wakubwa kama David Beckham na mkewe Victoria wakihudhuria.
Utakumbuka hadi kufikia sasa Marc Anthony ameshafunga ndoa nne na kujaliwa kupata watoto sita, huku wengine wawili akiwapata kati ya mwaka 1994 na 1995 ka-bla ya kufunga ndoa yoyote.
Mkali huyo wa Latin Music, alianza kwa kufunga ndoa na aliyekuwa Miss Universe 1993, Dayanara Torres kutokea Mexico hapo Mei 9, 2000, huko Las Vegas, Ma-rekani na kujaliwa watoto wawili, Cristian Marcus (2001) na Ryan Adrian (2003).
Hata hivyo, ndoa hiyo ilikuja kuvunjika Oktoba 2003, huku Dayanara akiomba talaka hapo Januari 2004. Ili kumsaidia kupona maumivu ya talaka hiyo, Dayanara alibad-ilisha pete yake ya ndoa na saa aina ya Cartier.
Kisha alikuja kumuoa mwanamuziki na mwigizaji, Jennifer Lopez (J.Lo) ambaye wa-lishirikiana kwenye muziki kwa kutumbuiza pamoja na kuigiza katika filamu, El Can-tante (2006).
Wawili hao walifunga ndoa Juni 5, 2004, na kufikia Februari 22, 2008 wakajaliwa kupata watoto pacha, Emme Maribel na Maximilian David ambao sasa wanaishi na mama yao.
Baada ya mafanikio katika ndoa na biashara, Aprili 9, 2012, Marc na J.Lo wali-tangaza kutengana. Marc aliwasilisha kesi ya talaka yao iliyokamilishwa Juni 16, 2014. Na Hadi sasa hii ndio ndoa ya Marc iliyodumu muda mrefu zaidi.
Na kufikia Novemba 11, 2014, huko La Romana, Jamhuri ya Dominika, Marc akafunga ndoa yake ya tatu na mwanamitindo Shannon De Lima kutokea nchini Venezuela. Lakini walitangaza kuachana mnamo Novemba 2016, na kumalisha mchakato wa talaka yao hapo Februari 13, 2017, huku wakiwa hawajafanikiwa kupata mtoto.